VINARA wa Ligi Kuu ya NBC na Mabingwa wa Kihistoria Tanzania bara Timu ya Yanga imeshindwa kutamba mbele ya watani zao Simba baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana mchezo wa Ligi uliopigwa uwanja wa Benjaman Mkapa jijini Dar es Salaam.
Hii ni Sare ya pili Mfulululizo msimu wa Ligi Kuu mpaka mwamuzi Ramadhan Kayoko anapuliza kipyenga cha mwisho Yanga na Simba zimegawana Pointi moja moja.
Kwa Matokeo hayo Yanga wamefikisha Pointi 55 na kuendelea kuongoza Ligi huku wakiwa wamecheza mechi 21 na kubakiwa na mechi 9 na Simba wamefikisha Pointi 42 nafasi ya pili huku wakiwa wamebakiwa na mechi 10 Ligi kumalizika.
0 Comments