ACT Wazalendo yalaani ‘Panya Road’

 Chama Cha ACT Wazalendo kimelaani vitendo vinavyofanywa na makundi ya vijana maarufu ‘Panya Road’ na kulitaka Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua stahiki za kulinda usalama wa raia na mali zao.

Kauli hiyo imetolewa baada ya siku za hivi karibuni ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam kuibuka vitendo vya uvamizi kwa wananchi na mali zao, kujeruhiwa na kuporawa matukio yaliyoripotiwa maeneo ya Chanika, Tabata na Kunduchi.

Kututokana na matukio ya kundi hilo kujenga hofu kwa jamii, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla Mei 2, 2022 alitangaza operesheni ya kukabiliana nalo ikiwa siku moja imepita tangu Rais Samia Suluhu Hassan kulionya kundi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 02/2022 na Chama hicho kupitia kwa Msemaji wa Kisekta Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarala Maharagande imesema vijana hao wamekuwa na desturi ya kuvamia nyumba moja baada ya nyingine na kutekeleza matukio hayo.

“Matukio hayo yamekuwa yakifanyika kati ya majira ya saa nne hadi saa tano mpaka sasa zaidi ya watu 89, wamejeruhiwa kwa mtindo wa kuingia nyumba moja baada ya nyingine.

“Wahalifu hao inasemekana wanafanya shughuli zao kwa uhuru mkubwa na huwa inawachukua hadi masaa mawili kufanya vitendo vyao huku vituo vikubwa vya polisi vikiwa karibu na maeneo ya matukio,”amesema

Chama hicho licha ya kulaani vitendo hivyo kimetoa ushauri kwa Jeshi hilo kufanya msako mkali wa wahalifu hao ili kuwabaini na kuwakamata na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Vikundi vya ulinzi shirikishi viimarishe usimamizi wake ili viweze kutekeleza kazi na wajibu wake kwa ufanisi na Jeshi la Polisi liwe na operesheni maalumu ya kudhibiti vitendo hivi vinavyohatarisha amani ya wananchi na mali zao,”amesema taarifa hiyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments