AU, EAC Wahimiza Uhuru wa Vyombo Vya Habari

Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) wameahidi kuendelea kishirikiana na vyombo vya habari katika nchi wanachama kuhakikisha uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari katika nchi zao.

Wakizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani (WPFD) ambayo yanaadhimishwa jijini Arusha leo Mei 3, 2022 wasema kuwa uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza ni mambo ya msingi.

Msemaji wa AU hapa nchini, Waynne Musabayana amesema suala la uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza ni suala la haki za binaadamu ambalo limeridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.

Musabayana amesema, AU utaendelea kufanya kazi na vyombo vya habari na kuwaunganisha wanahabari barani Afrika katika kubadilishana uzoefu.

"Katika maadhimisho haya tumefadhili waandishi wanne wamekuja hapa kishirikiana maadhimisho haya lengo ni kubadilishana uzoefu" amesema

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Stephene Mlote amesema Jumuiya hiyo kupitia nchi wanachama itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.

Hata hivyo amesema ni vyema vyombo vya habari kutimiza wajibu wake kwani hakuna uhuru ambayo hauna wajibu.

Mlote amepongeza jitihada za Rais Samia Suluhu katika kutangaza vivutio vya Utalii jambo ambalo limekuwa na manufaa makubwa kwa nchi zote wanachama wa Jumuiya hiyo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments