CCM MANYARA YAMMWAGIA SHAKA TUZO NA ZAWADI KIBAO

 

Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara  kimempatia tuzo mbalimbali Katibu wa NEC Itikadi Siasa na uenezi Shaka Hamdu Shaka kwa kutambua mchango na utendaji wake ndani ya Chama.   

Pamoja na tuzo, Ccm imempatia Ndugu Shaka Mafuta ya alizeti Lita 40,mbuzi na  zaidi ya kilo sitini za mchele kutoka Magugu.

Kuhusu usajili wa wanachama kuanzia januari mwaka huu Hadi Mwezi Mei, Katibu wa Ccm mkoa wa Manyara Naomi Kapambala amesema Mbulu imeongoza kwa  kusajili wanachama 7,869,wilaya ya Kiteto inafuatia ikiwa imeandikisha wanachama 4,930 huku Hanang ikishika nafasi ya tatu ikiwa imesajili takribani wanachama 2,273.
Aidha Waliokusanya ada za wanachama Hanang milioni mbili laki Saba na elfu ishirini kwa miezi mitano,Mbulu Milioni Moja na kiteto.

Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na uenezi Shaka Hamdu Shaka  yupo mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ambapo atazungumza na viongozi mbalimbali wa Chama ngazi zote.

Tazama Picha Na Za Matukio Mbali Mbali Za Katibu   wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ( CCM) Shaka Hamdu Shaka amewasili mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Katibu wa Chama hicho mkoa Naomi Kapambala.

Shaka ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Manyara baada ya kuwasili na kupokelewa atapokea taarifa ya CCM Mkoa hasa inayoelezea hali ya Chama pamoja utekelezaji wa Ilani pamoja  na taarifa ya Serikali Mkoa. Pia atatembelea miradi ya maendeo ambapo baadhi ya miradi imekamilika na mingine inaendelea.
 


Post a Comment

0 Comments