CCM Yampa ‘Tano’ Samia Kuongeza Mishahara, Kikokotoo

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ongezeko la mishahara kikiwemo kima cha chini kwa asilimia 23.3 na kupandishwa kwa malipo ya mkupuo ya pensheni kwa wastaafu.

Nyongeza hiyo ya mishahara imekuja baada ya watumishi kuisubiri tangu mwaka 2015.

Katika sherehe za Mei mosi mwaka huu zilizofanyika jijini Dodoma, Rais Samia aliwahakikishia wafanyakazi kuongeza mishahara na jana, Mei 14, 2022, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilisema Rais Samia ameridhia mapendekezo ya kuongeza mishahara.

Kutokana na ongezeko hilo, Serikali imepanga kutumia Sh9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kugharamia mishahara ya wafanyakazi.

Leo, Jumapili Mei 15, 2022 taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi wa (CCM), Shaka Hamdu Shaka imesema hatua hiyo ni mwendelezo wa hatua kadhaa zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kwa lengo la kuboresha maslahi na stahiki za wafanyakazi nchini.

“Uamuzi wa kupandisha mishahara, ikiwa ni pamoja na kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa asilimia 23.3  umefanyika kwa kuzingatia taratibu za mwenendo wa uchumi, pia ule wa kuelekeza kukamilishwa kwa taratibu za kisheria kuhakikisha malipo ya mkupuo ya wastaafu yanapandishwa kutoka asilimia 25 hadi asilimia 33,” imesema taarifa hiyo ya CCM ya kumpongeza Rais Samia na kuongeza: 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments