Chunya Kuwasaka Watoto Migodini

 Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imesema itaanza oparesheni ya kuwasaka na kuwaondoa watoto walioacha masomo na kujihusisha na ajira za utotoni kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chunya, Tamimu Kambona amesema hayo leo Jumatatu Mei 23,2022 ofisini kwake baada ya waandishi wa habari kuhoji kuwepo kwa kundi la watoto wanaojihusisha na ajira za utotoni kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo katika kata ya Sangambi wilayani humo.

Timamu amesema kumekuwepo na kundi kubwa la watoto wanaoacha masomo na kujihusisha na utafutaji wakiwa na umri mdogo licha ya kupiga marufuku wamiliki wa migodi kutoa ajira kwa watoto.

''Tulishatoa katazo kwa wachimbaji na wamiliki wa migodi  kutokana na ukubwa wa tatizo  hivyo tutaanza kunafanya zoezi la kuwasaka ikiwa ni pamoja na kuwaonya wazazi kutoruhusu  kwenda kufanya shughuli hizo na badala yake wapate fursa ya kupata elimu''amesema.

Amesema kuwa changamoto kubwa ya ajira za utotoni wazazi wanachangia kwa kutanguliza maslai ya fedha.

''Kama mnavyojua Halmashauri ya Chunya shughuli kubwa ni uchimbaji wa madini hivyo kuna watoto wengine wanatoka mikoa mbalimbali wanakuja kujitafutia rizki badala ya kupenda shule sasa ili kunusuru kundi hili ni kuwaondoa katika maeneo hayo hatarishi na kujua maeneo wanayotoka na kuwarejesha ili wapate haki zao za Msingi'' amesema.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya Simu Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Kasaka amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa  wachimbaji wadogo  kuachana na tabia ya kutoa ajira kwa watoto pamoja na kuwataka wazazi kubeba majukumu yao ya kutunza na kusomesha watoto .

 

Post a Comment

0 Comments