IKUNGI NI SALAMA KWA WAFUGAJI NA WAKULIMA

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ikungi leo tarehe 23/05/2022 imemaliza mgogoro baina ya baadhi ya wafugaji kutoka Mkundi mkoani shinyanga, iramba na Igunga dhidi ya wananchi wa kata ya Mwaru kijiji cha Mdughuyu

Akizungunza wakati wa kikao na wananchi hao Mkuu wa wilaya ya Ikungi *Ndugu Jerry C. Muro* amewataka wafugaji wahamiaji kutoingiza mifugo katika mashamba ya wananchi na badala yake kuelekeza mifugo yao katika ushoroba wa bonde la wembere ambalo baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya ufugaji

Dc Muro amesema tayari *Mheshimwa Rais. Samia Suluhu Hassan* alishatoa maelekezo maalum ya namna ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulma pamoja na wananchi na kusisitiza maelekezo ya Rais Samia yanapaswa kufuatwa na kuheshimiwa ili kuleta amani na usalama wa wafugaji pamoja na wakulima

Awali wananchi wa kitongoji cha shololi walizua taharuki kufuatia uwepo wa mifugo mingi kutoka maeneo ya shinyanga, iramba na igunga ambayo ilitishia uhai wa mashamba na maeneo yao ya asili ya kuchungia jambo lililosababisha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya ikungi kuweka kambi kutatua changamoto hiyo

Katika kikao hicho Diwani wa kata ya Mwaru Iddi Makangale pamoja na kushukuru hatua ya haraka iliyochukuliwa na uongozi wa wilaya ya ikungi kufika kwenye eneo la changamoto haraka amehaidi kusimamia maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuchunga na kulima pasipo kutengeneza migogoro
*Tazama picha za matukio* 👇🏾👇🏾




Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ikungi 23/05/2022
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments