KATIBU MKUU CCM AANZA ZIARA SIMIYU

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo amewasili mkoani Simiyu huku akipokewa na Viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa na Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.David Kafulila.


Ndugu Chongolo amepokewa njia panda katika Kata ya Isanga wilaya ya Maswa katika Jimbo la Maswa Magharibi, Simiyu leo Mei 31,2022 akitokea mkoani Shinyanga

Ndugu Daniel Chongolo ambae pia ni Mlezi wa Mkoa huo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu, ambapo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha na kuhimiza uhai wa chama kuanzia ngazi ya mashina.

Chongolo ambaye ameambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ngemela Lubinga pia atazungumza na wanachama wa Chama hicho pamoja na kukagua miradi ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya uchgauzi Mkuu mwaka 2020-2025.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments