MAANDALIZI YA MKUTANO WA 65 WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI-KAMISHENI YA AFRIKA YAANZA RASMI

Maandalizi ya mkutano wa 65 wa shirika la utalii Duniani- kamisheni ya Afrika (65 UNWTO-CAF) yameanza rasmi ambapo katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dkt Fransis Michael amezindua kamati ya maandalizi huku akiwasisitiza kuchukulia umuhimu na uzito jukumu walilonalo.

Dkt Fransis alisema kuwa wanasababu zote za kujivunia Tanzania kupata fursa ya kuandaa mkutano huo utakaofanyika tarehe 5 ha7 October ambao pia utatoa fursa ya kuitangaza nchi kwani utaleta watu wengi ambao watakuja kushuhudia yale yaliyotangwaza na Rais Samia Suluhu katika filamu ya Royal Tour hivyo ni vema wanakamati wakapangilia mambo yote mapema.

“Tumejaribu kutafuta watu kutoka katika nyanja, wizara zote katika kamati hii ili kusudi tuweze kuhakikisha kwamba maandalizi haya yanakuwa bora na yanafana na kuweza kufanya mkutano huu kuwa wa mfano,”Alisema Dkt Fransis.

Alifafanua kuwa majukumu makubwa ya kamati hiyo ni kuandaa mkutano ambapo wanatakiwa kuandaa uweze kufana na kuwa kivutio kikubwa Kuvutia watu wa nje na mataifa mengine kuja kutembelea nchi ya Tanzania.

“Tunatakiwa tuhakikishe kuwa kamati inafanya kazi kwa weledi kwasababu mkutano huu ni wa kimataifa, tunaleta viongozi wa nchi na nchi zingine hivyo ni lazima tuhakikishe Tanzania tunakuwa mfano wa nchi zingine,”Alieleza.

Kwa upande wake Felex John mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo kutoka Tanzania bara ambaye pia ni kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii alisema kuwa tukio hilo wanalichukulia kimkakati kwasababu ni tukio ambalo linakwenda kuleta wageni wengi katika nchi.

“Ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo wa mkakati wetu wa utalii mikutano ambao unalenga watalii wengi na wegeni kuja katika nchi yetu kwahiyo kama mnavyofahamu mkutano huu utakunisha mawaziri wanaosemamia sekta ya utalii na uhifadhi kutoka nchi zote barani Afrika lakini pia watakuja na watu wengi hivyo wadau wetu muhimu wa sekta ya utalii wajiandae kupokea idadi kubwa ya wageni kutoka mataifa yetu ya Afrika,” Alisema Felex John.

Naye mwenyekiti mwenza kutoka Tanzania Zanzibar Rahim Bhaloo alisema kuwa Tanzania imejifungua katika sekata ya utalii, Rais Samia Suluhu ameitangaza sana vivyo hivyo na Rais Hussein Mwinyi ambapo ni fursa kwa Tanzania kujiuza kwa dunia kwa kujitangaza na kuonesha vivutio.

Aliongeza kuwa huu ni muda mzuri wa kushirikiana kwa pamoja fursa zilizopo katika sekta ya utalii ili kujiletea maendeleo kama nchi

Katibu Mkuu wizara ya maliasili na utalii Dkt Francis  Michael akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Arusha(hawapo pichani)juu ya maandalizi ya mkutano wa 65 wa shirika la utalii Dunia
Mwenyekiti mwenza kutoka Tanzania Zanzibar Rahim Bhaloo akizungumza na vyombo vya habari
Na Pamela Mollel,Arusha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments