MADIWANI IKUNGI WATAKIWA AJENDA YAO KUBWA IWE NI KUKUSANYA MAPATO

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Ally Mwanga (katikati) akiongoza kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi wilayani humo juzi na jana.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya Mkiwa Stephen Mtyana na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Justice Kijazi.

Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo Jovison Ntangek akitoa salamu za Serikali katika kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo. Kulia ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendegu na Mchumi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

Baadhi ya watendaji wa Kata, Vijiji na Watumishi wa wilaya hiyo wakiwa kwenye baraza hilo.

Baraza likiendelea.

Baraza likiendelea.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye baraza hilo.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo.

Kikao kikiendelea.

Diwani wa Kata ya Muhintiri Hamisi Mpuma akitoa taarifa ya mapato ya kata hiyo.

Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Maki akichangia jambo kwenye baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Mungaa Dulle Gabriel Theodor akichangia jambo kwenye baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Isuna Stephano Missai akizungumza kwenye baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Ntuntu, Omari Toto akitoa taarifa ya mapato kwenye baraza hilo.

Diwani wa Viti Maalum, Hellena Petro akisisitiza umuhimu wa ukusanyaji mapato Kata ya Tuntu.

Diwani wa Viti Maalum kutoka Kata ya Irisya, Subira Kitiku akitoa taarifa ya mapato.

Diwani wa Viti Maalum Pili Kigwanda kutoka Kata ya Ihanja akisoma taarifa ya mapato.

Wadau kutoka Taasisi ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Omari Hamisi.

Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale akichangia jambo kwenye baraza hilo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Sophia Kizigo akizungumza wakati akitoa salamu za Serikali.

Taswira ya baraza hilo.

Baraza likiendelea.

Baraza likiendelea.


Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Wilaya ya Ikungi, Faraja Maliga akitoa taarifa kwenye baraza hilo.


Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Jovison Ntangek akimkabidhi funguo wa pikipiki Afisa Mtendaji wa Kata ya Mgungira, Abdallah Simon kwa kuwa mshindi wa kukusanya mapato ya zaidi ya Sh.157 Milioni.

Zawadi kwa washindi wengine wa ukusanyaji mapato zikitolewa. Anayepongezwa kushoto ni Afisa Mtendaji Kata ya Muhintiri, Bahati Mkungile.


MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wametakiwa ajenda yao kubwa kuwa ni ukusanyaji wa mapato ili wilaya hiyo iweze kupaa kiuchumi.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ally Mwanga wakati akiongoza kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi wilayani humo jana na leo.


Mwanga alisema halmashauri yoyote haiwezi kupiga hatua ya maendeleo bila ya kuwa na mapato ya kutosha hivyo madiwani wanakila sababu ya kuwa mstari wa mbele katika kukusanya mapato kwenye maeneo yao.

" Ninyi madiwani ndio tunaowategemea kwa kiasi kikubwa kuhamasisha ukusanyaji wa mapato kwenye kata zenu kwani huko ndiko chimbuko la mapato hivyo ni jukumu lenu kuongeza bidii ya ukusanyaji kwa kushirikiana na watendaji wenu wa kata" alisema Mwanga.

Alisema hivi sasa ajenda yao kubwa iwe ni kukusanya mapato tena kwa nguvu zao zote ili halmashauri hiyo iwe kinara kwa kukusanya mapato hapa nchini.

Katika hatua nyingine Mwanga alimuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Justice Kijazi kuifumua idara ya afya kutokana na kuwa na changamoto nyingi za kiutendaji kutokana na baadhi ya watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kwa mazoea hivyo kukwamisha mambo mengi.

"Mkurugenzi nakuagiza ifumue idara ya afya kwa kuwabadilisha vituo watendaji wake, waliopo hapa wilayani wapeleke huko vijijini na wale wenye uwezo waliopo vijijini walete hapa wilayani itasaidia kurudisha uwajibikaji na kupunguza haya malalamiko ya kila siku ambayo yanaichelewesha kimaendeleo halmashauri yetu" alisema Mwanga.

Hata hivyo Kijazi alieleza kwamba changamoto hiyo itamalizika hivi karibuni kwani wanategemea kumpata mganga mkuu wa wilaya baada ya wa awali kuhama na nafasi hiyo kushirikliwa na kaimu."Maagizo yako nimeyapokea lakini tunategemea kumpata mganga mkuu wetu hivi karibuni naamini changamoto hii itakwisha mara baada ya kufika" alisema Kijazi.

Akiongelea kuhusu ukusanji wa mapato Kijazi alisema itakuwa haina maana ya kukusanya mapato mengi na matumizi yake yakawa makubwa ambapo alitoa wito kwa watendaji kuzingatia jambo hilo ili kuyalinda mapato hayo.

Alisema mapato ndio injini ya halmashauri hivyo ni jukumu la kila mmoja wao kuhakikisha yanakusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali kwani ndiyo yanayosaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika baraza hilo madiwani walipata fursa ya kutoa taarifa mbalimbali ya matumizi ya fedha katika miradi na kujadiliana mbinu za ukusanyaji wa mapato huku kata vinara kwa ukusanyaji mapato zikipongezwa huku zile ambazo zilionekana kushuka kimapato zikitakiwa kuongeza bidii kwa kujifunza kutoka kwa zile zilizofanya vizuri.

Aidha watendaji wawili wa kata mbili zilizoongoza kwa ukusanyaji wa mapato walizawadiwa pikipiki kila mmoja huku wengine wakipatiwa fedha taslimu ikiwa ni motisha na kuwapa ari ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.

Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Kizigo akizunguza wakati akitoa salamu za Serikali aliwaomba waratibu wa zoezi la Sensa ya watu na makazi kuwahimiza watendaji wa vijiji na vitongoji kutangaza nafasi za kuomba ajira ya muda ya ukalani na usimamizi wa zoezi hilo huku akiwaomba watoe kipaumbele kwa vijana wenye sifa wa wilaya hiyo kabla ya kuwachukua wale wanaotoka nje ya wilaya hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments