Magunia 100 ya mkaa yakamatwa hifadhi ya Kigosi

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) wamekamata zaidi ya magunia 100 ya mkoa ambayo inadaiwa kuwa miti iliyokatwa na kuchoma mkaa huo imetoka ndani ya Hifadhi ya Taifa Kigosi.

Shehena hiyo imekamatwa kitongoji cha Namsega kata ya Runzewe Magaribi wilaya ya Bukombe mkoani Geita na wakuu wa hifadhi ya Taifa Kigosi wakiongozwa na mkuu wa hifadhi hiyo, Vitalis Peter wakati wakielekea kijiji cha Namsega kwa lengo la kuelimisha wananchi umuhimu wa uhifadhi na kutunza mazingira ya pembezoni mwa hifadhi hiyo.

 "Hapa hakuna mti uliokatwa hivi karibuni isipokuwa hapa ni kijiwe cha kukusanyia mkaa unaotoka ndani ya hifadhi ya Kigosi na kuja kupakiliwa kwa ajili ya kusafirisha hivyo kuazia sasa gari halitaodoka hadi mfanyabiashara wa mkaa atakapo patikana na kuonyesha anapo vuna miti ya kuchoma mkaa", amesema 

"Hata vibali vina makosa hivyo nitaacha askari wangu hapa kulinda gari hadi kieleweke hatukubaliani na uharibifu huu mutu anadaganya anaeneo la kuvuna miti na kuchoma mkaa kumbe anafanya uhalibifu ndani ya hifadhi ya Taifa Kigosi", amesema Peter.

Msaidizi wa mfanyabiashara wa mkaa huo, Daudi Peter (32) amesema hawajavuna miti ndani ya hifadhi huku akibainisha kuwa wanavuna katika eneo ambalo wamepewa kibali na mamlaka za Kijiji na TFS.

Hata hivyo, Peter alikikimbia baada ya kuulizwa maswali na viongozi hao.

Dereva wa lori lililokamatwa na shehena hiyo ya mkaa, Masele Lujiga amesema yeye amekuwa akikodiwa na mfanyabiashara huyo kubeba mkaa kutoka eneo ambalo limeandaliwa kwenda Mwanza.

Kwa mjibu wa mkazi wa kijiji hicho ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, amedai kuwa magunia ya mkaa yanatoka ndani ya hifadhi yakisomwa na mikokoteni ya ng'ombe usiku mpaka kwenye kituo ambacho magari hufika kuchukua.

  Na Ernest Magashi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments