Makinda: Marufuku Maofisa Kuomba Fedha Ruhusa Ukarani Wa Sensa

KamisAa wa Sensa, Anna Makinda amesema ni marufuku Kwa Maofisa wa Serikali kuwaomba  fedha waajiliwa wao pindi wanapoomba ruhusa ya kutaka kwenda kuomba ukarani wa sensa.

Marufuku hiyo ameitoa leo Mei 12, 2022 katika kikao cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikalini kinachofanyika jijini Tanga.

Makinda amesema sensa ni muhimu kwa Tanzania na ni kosa kisheria kuwaomba pesa makarani

"Ni marufuku kutoa pesa kisa kazi ya ukarani, waajiri acheni tabia hiyo na nyie waombaji msishawishike kutoa pesa kwa mtu yeyote kwa kuwa maombi hayo yanakwenda kitehema na hakuna gharama yoyote" amesema Makinda.

Kamisaa huyo amesema watendaji wa vijiji na kata hawaruhusiwi kuomba nafasi hiyo kwa kuwa wao watakuwa sehemu ya usimamizi wa mchakato huo.

Sensa inafanyika Agosti 23, 2022.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments