Mhata ameyasema hayo wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2022/2023.
Amesema kata ya Nandete wilayani Nanyumbu kulikuwa na mradi mkubwa wa maji ambao ulichezewa.
“Nilikuomba ulete wakaguzi, watu wamechakachua ule mradi, mradi umetumia fedha nyingi lakini hautoi maji ya kutosha. Hatutakubali fedha za Serikali za walipa kodi watu wachache wananufaika,” amesema.
Aidha, Mhata amesema katika kata ya Mnanje kuna mradi wa Benki ya Dunia (WB) ambao tangu umezinduliwa haujawahi kutoa hata ndoo moja ya maji.
“Naomba waliohusika na ule ubadhirifu wachukuliwe hatua. Hili jambo halikubaliki, muda wa kuchezea maji, wakuchezea fedha za miradi ya maji ndani ya wizara yako mbele yaw ewe (Waziri) muda umekwisha,”amesema.
0 Comments