Mchakato Kuwahoji Kina Mdee waanza

Mchakato wa kuwahoji wabunge 19 wa viti maalumu umeanza rasmi katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Baraza Kuu la Chadema linaendelea likiwa na ajenda saba ikiwemo kujadili rufaa za wabunge hao.

Wabunge hao ni pamoja na Halima Mdee  Grace  Tendega,  Agnesta Lambet,  Jesca Kishoa, Ester Bulaya, Ester Matiko, Salome Makamba, Nusrat Hanje, Tunza Malapo, Conchestar Rwamlaza, Naghenjwa Kaboyoka, Hawa Mwaifunga, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Asia Mohammed.

Wengine ni Sophia Mwakagenda, Cecilia Pareso, Kunti Majala na Felister Njau, ambao kwa pamoja  walivuliwa nyadhifa za uongozi na uanachama mwaka 2020 baada ya kubainika kwenda kinyume na msimamo wa Chadema kula kiapo cha kuwa wabunge wa viti maalumu bila baraka za Chadema.

Hata hivyo, licha ya kufukuzwa uanachama, wamekata rufaa katika baraza kuu la chama hicho lenye wajumbe 437 ambao kikao chake kinaendelea hivi sasa kikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments