PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AKIWA ZIARANI MKOANI SHINYANGA

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wananchi wa Shina namba 3, Tawi la Ntobo A ikiwa ni mkutano wa kwanza wa shina hilo lililopo Kata ya Ntobo, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

wananchi wa Shina namba 3, Tawi la Ntobo A wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chingolo (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kwanza wa shina hilo lililopo Kata ya Ntobo, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Wanachama wengine wakifurahia baada ya kuwekwa jiwe la Msingi katika jengo hilo
Wananchi wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo alipokuwa akiwahutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la chama hicho Kata ya Isaka.

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka Kwa Mganga Mkuu Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga,Dkt Ernest Chacha, inayojengwa katika Kijiji Cha Ntobo A kata ya Ntobo ambapo serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.74 kukamilisha ujenzi huoKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka Kwa Mganga Mkuu Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga,Dkt Ernest Chacha, inayojengwa katika Kijiji Cha Ntobo A kata ya Ntobo ambapo serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.74 kukamilisha ujenzi huo.Chongolo yuko katika ziara ya siku 9 akikagua uhai wa chama na miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na serikali kupiitia ilani ya CCM ya mwaka 2020- 2025,

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Shina namba 3, Tawi la Ntobo A Ndugu John Herman Maige wakati wa mkutano wa kwanza wa shina hilo lililopo Kata ya Ntobo, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Wananchi na Wanachama wa chama cha CCM wa Shina namba 3, Tawi la Ntobo ,kata ya Ntobo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri nyumbani kwa Mwenyekiti wa Shina namba 3, Tawi la Ntobo A Ndugu John Herman Maige

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiondoka kwa Mwenyekiti wa Shina namba 3, Tawi la Ntobo A la Ndugu John Herman Maige (njano) alipomaliza mkutano wake kwanza wa shina hilo lililopo Kata ya Ntobo, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo alionesha jambo ndani ya jengo alipokwenda kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Isaka ambacho kimejengwa kwa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 50 zilizotolewa na Serikali awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Sofia Mjema.
 

Katibu Mkuu wa CCM Ndubu Daniel Chongolo akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe.Iddi Kossi Iddi kabla ya kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Isaka ambacho kimejengwa kwa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 50 zilizotolewa na Serikali awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Sofia Mjema.
Sehemu ya muonekano wa kituo cha Afya cha Isaka kwa sasa
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Isaka wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo alipokuwa akizungumza na Wananchi hao alipokwenda kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Isaka ambacho kimejengwa kwa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 50 zilizotolewa na Serikali awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Sofia Mjema.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments