Rais Samia Aitisha Kikao Cha Dharura Usiku, Atoa Agizo

Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza mawazi, makatibu wakuu wa baadhi ya Wizara kutafuta suluhisho la haraka la kukabiliana na tatizo la kupanda bei ya mafuta nchini.

Mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo baada ya kuitisha kikao cha dharura kilichofanyika usiku wa kuamkia leo Mei 9, 2022 Ikulu ya Dar es Salaam cha kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta ya ptroli, dizeli na mafuta ya taa nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria katika kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, makatibu wakuu wa wizara hizo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.

Rais Samia ameitisha kikao hicho ikiwa zimepita siku tatu tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa naye alipoitisha kikao na baadhi ya mawaziri kufanya tathmini ya bei ya mafuta na kuangalia namna gani Serikali inaweza kufanya ili kupunguza athari ya bei ya mafuta na kuleta unafuu wa gharama za maisha kwa Watanzania.

Katika kikao chake Waziri Mkuu kilichofanyika usiku wa kuamkia leo Alhamisi Mei 5, 2022 jijini Dar es Salaam, Majaliwa alisema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Kikao hicho ambacho nacho kilifanyika usiku kiliwahusisha baadhi ya mawaziri wakiwamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati, January Makamba, Makatibu Wakuu, pamoja na watendaji wakuu wa taasisi za EWURA, TPDC na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments