Rais Samia Awataka Waandishi Kuzingatia Mila, Desturi Za Kiafrika


 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka waandishi wa habari kuandika habari kwa kutunza na kuheshimu mila na desturi za kiafrika.

Akuzungumza leo Jumanne Mei 3, 2022 katika maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani ambayo kitaifa imefanyikia jijini Arusha, Rais Samia amesema kukopa mila na desturi husababisha migongano isiyo ya lazima.

"Uhuru wa habari hauchagui mipaka hivyo pamoja na hilo waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia mila na desturi za kiafrika kuandika mazuri ikiwemo vivutio vyote vilivyomo," amesema Rais.

Amesema ni vyema wakaandika habari ka kuthamini rasilimali zilizopo Afrika ni vyema kujivunia rasilimali mlizonazo pamoja na kuzilinda.

UNESCO yaridhishwa na uhuru wa habari nchini

Katika maadhimisho hayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeeleza kuridhishwa za ukuaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini na uhuru wa kujieleza.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi mkazi wa UNESCO Kanda ya Afrika ya Mashariki, Profesa Hubert Gijzenz amesema Tanzania ilistahili kuandaa maadhimisho haya ambayo yameshirikisha wahabari kutoka mataifa 54 barani Afrika.

Amesema UNESCO itaendelea kuthamini mchango mkubwa wa vyombo vya habari duniani katika kusaidia jamii katika masuala mbalimbali.

Amesema wakati wa ugonjwa wa Uviko-19 wanahabari wamefanya kazi kubwa sana kuhabarisha watu kuhusu ugonjwa huo.

Hata hivyo amesema wanahabari duniani bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo kupata madhara wakiwa kazini ambapo tayari wanahabari 55 mwaka jana wamefariki.

Amesema hivi sasa ambapo kuna matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii ambayo hata hivyo, baadhi vimekuwa vikiwafanyia ukatili wa kuwadhalilisha wanawake.

Amesema katika vyombo vya habari kati ya wanahabari 10 saba kati yao wamefanyiwa ukatili.

Ametaka kukomeshwa matukio ya ukatili kwa waaandishi wa habari wanawake

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments