Recent-Post

RC SINGIDA AFUNGUA TAMASHA LA MICHEZO LA WANAFUNZI WA TAASISI YA UHASIBU SINGIDA

 


Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akizungumza jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati akifungua wiki ya michezo ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida iliyoanza juzi mkoani hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa wiki hiyo ya michezo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akipiga mpira wakati wa ufunguzi huo.


Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo. Kulia ni Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dk.James Mrema.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akikagua timu katika ufunguzi huo.

Mazoezi ya viungo yakifanyika.

Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea siku ya kwanza ya tamasha hilo la michezo.

Mazoezi yakifanyika.

Jogging ikifanyika.

Mashabiki wakifuatilia michezo iliyokuwa ikifanyika.

Michezo ikiendelea.

michezo ikiendelea.

Kivumbi kikitimka wakati wa michezo hiyo.


Mazoezi yakifanyika.

Timu zikiingia uwanjani.

Picha ya pamoja.

Mchezo wa Netball ukifanyika.

Mgeni rasmi DC wa Mkalama Sophia Kizigo (kulia) akiwasili kufungua michezo hiyo.

Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

Timu zikiwa uwanjani.
Ukaguzi wa timu ukifanyika.
Picha ya Pamoja

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imeanza rasmi wiki ya michezo huku ikitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa umma wa watanzania na vijana waliohitimu kidato cha nne mwaka 2021 na miaka ya nyuma kujiunga na taasisi hiyo kwa ajili ya masomo kwa ngazi ya cheti yaani Certificate na Diploma kwa mwaka 2022/2023 baada ya Taasisi hiyo kufungua dirisha la maombi.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa. William Amos Pallangyo Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dk. James Mrema alisema nafasi hizo zipo na akawaomba vijana kuzichangamkia.

Awali akifungua michezo hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo aliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutumia michezo hiyo kupata fursa mbalimbali za kuwainua kiuchumi na sio kuwa "memory card'

"Tumieni michezo kama sehemu ya kuwaleta pamoja kutambua na kupata fursa mbalimbli zilizopo kwenye jamii ili muinuke kiuchumi na si kuwasindikiza wenzenu kwani kupitia michezo itawasaidia kuzitambua fursa mbalimbli zikiwemo za kiuchumi " alisema Kizigo.

Dkt. Mrema akizungumzia tamasha hilo alisema litafanyika kwa wiki nzima ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali kama mpira wa pete, mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, mchezo wa bao.Pia kutakuwa na shughuli za kuinua vipaji kwa kutafuta MISS na MR tia, waimbaji, wachekeshaji, waigizaji, wacheza muziki na ngoma, watanashati, wabunifu, wasiriamali.

Alisema kuwa vilevile kutakuwa na maonyesho ya wajasiriamali mbalimbali wa ndani na nje ya Taasisi na kuwa hiyo kwao ni fursa kubwa kwa wanafunzi wao na jamii nzima inayowauzunguka ambapo siku ya kilele cha Tamasha hilo ambayo ni Jumamosi ya Mei 21,2022 zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi mbalimbali.

Dk. Mrema alitumia nafasi hiyo kuipongeza TIA kwa kuweka wiki hiyo ya Tamasha la Michezo kwani inawaongezea wanafunzi wao uelewa wa maisha kwamba si elimu tu inayoweza kukufanikisha katika maisha ni wazi kazi na dawa ndio njia pekee ya mafanikio.

Alisema kusoma kunahitaji kucheza ili uweze kuelewa na si kucheza pekee ila kujishughulisha na shughuli zingine ili kutanua ubongo, kulinda na afya ya kiakili ili kutia chachu katika kupambana mawazo hasi na kuruhusu kuwaza katika mlengo chanya.

Pia alisema michezo ni kukuza ushirikiano na urafiki kwani michezo hunoga pale mnapokuwa wengi na kujumuika kwa pamoja, Hii inamaana kwamba kidole kimoja hakivunji Chawa.

Alisema michezo huwalinda wao na wengine waliokaribu nao kiafya, kiakili, kimwili na kuwa michezo inaweza kutumika kama njia bora sana katika kujikinga na maradhi mbalimbali na kuokoa kipato kinachoweza kutumika katika ununuzi wa madawa ya kujitibu na zaidi ya yote ni lazima wajikite katika kukuza vipaji vya wanafunzi na wasipojua vipaji hivyo ni dhahiri wanaweza kujikuta yanawapata kama wale watu waliopewa talanta katika Biblia, Mathayo 25:14-30 ambao waliozitumia talanta zao walipata zingine aliyeificha hakupata kitu chochote.

"Tunapenda kuishukuru nchi yetu kwani toka enzi za mababu imekuwa ikijitahidi kuhakikisha wananchi wanajihusisha na michezo kwani hii husaidia katika ulinzi na usalama, kuzuia kutenda uhalifu, kuongeza ajira, kupunguza matumizi ya changamoto za kiafya nakadhalika hakika uhuru huu tulionao ndio pekee unaoturuhusu kupata nafasi ya kuweza kujikita katika shughuli hizi za maendeleo na tunaipongeza Serikali hii kwa dhati kwani Amani, Utulivu, iliyopo ni fahari kubwa sana kwetu na vizazi vyetu' alisema Mrema.

Aidha Dk.Mrema alisema katika wiki hii ya michezo TIA kwa mwaka 2022 wanajivunia furaha waliyonayo japo kuwa kuna mambo kadhaa ambayo wanayatamani kama kuweka viwanja vya michezo vya kisasa ambavyo vitaamsha hari za wengi kujihusisha na michezo,kuweka uzio kuzunguka Taasisi hiyo ili kulinda maeneo yao na wanafunzi kwa ujumla katika changamoto mbalimbali wanazozipitia, kuongeza mabweni ya kisasa katika iddi kubwa ambayo itaweza kuwasaidia wanafunzi kujiingiza katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa wanakaa mtaani, kuwakinga wanafunzi katika maambukizi mapya ya magonjwa ya zinaa na VVU na UKIMWI.

Alitaja mambo mengine wanayoyatamani kuwa ni kuwakinga wanafunzi katika kujiingiza katika madawa ya kulevya na tabia hatarishi, kutumia mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na wadau wengine kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi ambao hawana uwezo kuweza kusomeshwa na kujikwamua katika janga la umaskini, kuwasaidia wanafunzi kupata ajira mbalimbali za muda mfupi na mrefu ili kuweza kupata fursa wakipambana na maisha.

Akizungumzia namna ya kujiunga na masomo katika chuo hicho kwa Mwanafunzi mwenye ufaulu kuanzia alama D4 anaweza kutuma maombi yake kwani atakuwa amekidhi sifa za kujiunga na dirisha liko wazi tangu Mei 14 hadi 15 Agost 2022.

Alisema wanawakaribisha kujiunga na programme za fani ya Uhasibu na Fedha, Uhasibu wa Umma, Ugavi na manunuzi, usimamizi rasilimali watu, masoko na uhusiano wa umma, usimamizi wa biashara. Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti yetu ya tassisi yaani www.tai.ac.tz au wanaweza kufika chuoni na kujaza fomu hizo. Pia wanaweza kupata fomu hizo katika shuile za sekondari walikohitimu kidato cha nne na kuwa wanawahakikishia kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania inatoa elimu bora yenye ujuzi wa maarifa na vitendo hivyo kumjengea mhitimu weledi na uwezo mkubwa wa kujiajiri na kuajiriwa.

Post a Comment

0 Comments