Saido Ntibazonkiza Amaliza Mkataba Yanga, Wamtakia Mafanikio Mema

Baada ya vuguvugu la kuwasimamisha Wachezaji wake wawili, rasmi Young Africans SC wameachana na Kiungo Mshambuliaji, raia wa Burundi, Saido Ntibazonkiza baada ya Mchezaji huyo kumaliza mkataba na Klabu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Yanga SC kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii imeeleza kuwa Ntibazonkiza amemaliza mkataba huo Mei 30, 2022 ikiwa ni kipindi cha miaka miwili cha utumishi wake ndani ya Klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Yanga SC imemshukuru Mchezaji huyo na kumtakia kila la kheri na mafanikio mema katika majukumu yake ya uchezaji Soka akiwa nje ya timu ya Yanga SC.

Hivi karibuni, Saido Ntibazonkiza na mwenzake Dickson Ambundo walisimamishwa kwa muda kwa madai ya utovu wa nidhamu baada ya kutoka nje ya Kambi hiyo na kuchelewa kurudi, wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wake wa Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Simba SC jijini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments