Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira Ya Wanahabari

Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya kazi kwa wanahabari nchini.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Mei 2, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Technolojia ya Habari, Dk Jim Yonaz katika warsha kya uelekea maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) jijini Arusha.

Amesema Wizara hiyo imekuwa na ushirikiano mkubwa na wanahabari ikiwa ni pamoja na kujenga, sekta hiyo na kuboresha pale penye mapungufu kwa maslahi ya nchi.

Akizungumza matumizi ya kidijitari, Dk Yonaz amesema ujio wa ulimwengu wa Kidigital unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi.

"Watendaji wote wa Wizara wako bega kwa bega katika kuboresha changamoto zote zilizopo katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira bora kwa wanahabari lengo likiwa kuinua uchumi wa nchi" amesema

Waandishi wa habari na wadau wa habari wa hapa nchini na kutoka mataifa kadhaa barani Afrika wanashiriki katika maadhimisho ya WPFD jijini Arusha ambapo kilele chake ni kesho.

Post a Comment

0 Comments