SHAKA ATAKA WANANCHI WAPEWE NAFASI YA KUSHUHUDIA UTEKELEZAJI WA MIRADI

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amewataka viongozi mbalimbali wanaofanya ziara hususan katika miradibya maendeleo kuwapa fursa wananchi kuona kinachofanywa na serikali.

Shaka ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipotembea soko Kuu la Kariakoo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, likiwemo Soko la Kariakoo alikoshuhudia hatua nzuri za ukarabatibwake.

"Ndugu zangu viongozi nadhani sasa ni muda mwafaka kubadilika katika hizi ziara, badala ya kukaa na kujifungia na kuzungumza sisi wenyewe, ni vyema tukawapa nafasi wananchi kuona Yale yanayofanywa na serikali yao chini ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema.

Shaka ameipongeza serikali kwa kazi nzuri inayofanya katika ujenzi nabukarabati wa soko hilo ambapo amesema litakapokamilika manufaa yake hayatakuwa kwa Kariakoo pekee bali ni kwa Dar es Salaam na Afrika Mashariki yote.

Awali akimkaribisha Shaka, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Ila, Ludigija Ng'wilabuzu, aliwapongeza wakandarasi wa mradi huo kwa kuutekeleza kwa kasi.

Amesema mradi huo upo chini ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo amesema kazi inaendelea vizuri na anaamini itakamilishwa katika muda muda wa makubaliano.




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments