SHAKA KWA WANANCHI MKOANI LINDI, APOKEA TAARIFA MABILIONI YA FEDHA YALIVYOTUMIKA KATIKA KULETA MAENDELEO

 KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amewasili mkoani Lindi ambapo pamoja na mambi mengine amepokea taarifa ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetumia mabilioni ya fedha yaliyotolewa na Seriakli ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Shaka amewasili katika Mkoa wa Lindi leo Mei 29 mwaka 2022 kwa ajili ya ziara kikazi inayoambana na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama pamoja na uhai wa Chama hicho.

Akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Mkoa wa Lindi Shaka amesema amefurahishwa na mapokeozi ya kihistoria aliyoyapata kwenye mkoa huo na atahakikisha analipa deni hilo kwa kuendeelea kuwapigania.

“Niwahakikishie ndugu wananchi Serikali hii inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan haitawaacha kinyonge na itaendelea kutoa mabilioni ya fedha kwa ajli ya miradi ya maendeleo,”amesema Shaka na kusisitiza Serikali ya Awamu ya Sita imetoa Sh.bilioni 52 za maendeleo kwenye mkoa huu.

Akizungumzia taarifa ambazo amepokea kutoka kwa viongozi wa Mkoa wa Lindi Shaka amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.“Nawapongeza kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imefanyika katika mkoa huu.”

Kuhusu kero ambazo zimetolewa na wananchi wa Mkoa wa Lindi, Shaka amesema amefarijika kuona wnanchi wakitoa kero na kisha kupatiwa ufumbuzi ambazo zimekuwa zikiwatatiza na kupata majibu na yale yanayohitaji muda yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.

Ametumia nafasi hiyo kuwahakikihsia wananchi kwamba Seriakli ya Rais Samia itaendelea kuwatumikia katika kuleta maendeleo. “Bilioni 52zimeletwa katika Mkoa wa Lindi kwa ajili ya maendeleo na kuja kwa fedha nyingi kiasi hiki haijawahi kutokea huko nyuma, ni Serikali ya Rais Samia imeleta fedha hii.

“Lindi ya leo hii ni tofauti na ile ya zamani, maendeleo yapo na mageuzi yamefanyika, wananchi wamekiri ndani ya mwaka mmoja Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa.Niwaombe msiwe wanyonge, Serikali ipo na Rais wetu yupo.Yale ambayo yanaonekana kama changamoto yafanyiwe kazi,”amesema Shaka.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Hamida Sharifu ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani za wananchi wa Mkoa huo kwa Raisa Samia Suluhu Hassana kwani katika kipindi cha mwaka mmoja ametoa fedha nyingi za maendeleo.

“Tumepokea fedha nyingi za maendeleo kwa ajili ya Lindi, kila eneo leo hii ujenzi unaendelea.Katika elimu kwa mapenzi makubwa ya Rais wetu Samia tumepokea Sh.bilioni 3.5 ambazo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ya elimu kwenye sekta hiyo.Tumepokea Sh.bilioni 4.5 kwa ajili ya sekta ya afya, tumepokea Sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Lindi.

“Rais anaupendo mkubwa kwetu na katika kila sekta kuna fedha tumepokea. Tumepokea milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa zanati.Tunajenga hospitali ya Mkoa wa Lindi na Sh.bilioni nne zimetua tayari.

“Kwenye sekta ya maji nako tumepokea fedha , tumepokea Sh.bilioni nane na mwaka huu tumepokea Sh.bilioni 3.5 kwenye sekta hiyo hiyo ya maji,”amesema na kufafanua kwa ujumla wamepokea Sh.bilioni 52 kwa ajili ya maendeleo na fedha hizo zote ni katika kipindi cha mwaka mmoja tu wa Rais Samia.

Awali akipokea taarifa ya CCM Mkoa wa Lindi, Shaka ameelezwa ambavyo uhai wa Chama umeimarika kwa kiasi kikubwa na kuhusu mchakato wa uchaguzi wa ndani ya Chama hicho umekwenda vizuri na hadi sasa hakuna dosari ya aina yoyote.





















TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments