Shirika La Umeme Tanzania Limezindua Mfumo Mpya Wa NIKONEKT APP Kwaajili Ya Kutoa Huduma Kwa Wateja Kwa Njia Ya Kidijitali

Shirika la umeme Tanzania limezindua mfumo mpya wa NIKONEKT APP kwaajili ya kutoa huduma kwa wateja kwa njia ya kidijitali
Akizungumza hivi karibuni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha Mhandisi Herini Mhina katika semina ya siku moja ya kuwapa uelewa wakandarasi juu ya mfumo huo

Alisema kuwa kupitia mfumo huo wa kidijitali utakwenda kuondoa changamoto mbalimbali na za mda mrefu ambazo zilikuwa zikiwakabili wateja

"Kwa mfumo ulivyo utaongeza uwazi zaidi na kutatua kero za vishoka ambao walikuwa wakisumbua wateja na kusababisha hasara kubwa "Alisema Mhandisi Mhina

Aliongeza kuwa kwa namna mfumo unafanya kazi utakwenda kumrahisishia mteja kufanya huduma akiwa nyumban kwa tumia simu ya mkononi


Kwa upande wake meneja wa EWURA Lorivil Longidu alipongeza shirika hilo kwa kuja na ubunifu mkubwa wa kuanzisha mfumo huo ambao utakaokwenda kutatua changamoto za wateja

Alisema kuwa kazi zote za ufundi wa umeme zitafanywa na wakandarasi au watu wenye leseni za EWURA

Na Pamela Mollel,Arusha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments