SIMBA SC YAENDELEA KUTOA DOZI LIGI KUU, YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0

 

MABINGWA Watetezi Simba wamezidi kuendelea kuipa presha Yanga kwenye mbio za Ubingwa baada ya kulipa kisasi cha mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya NBC katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba walipata bao dakika ya 13 kupitia kwa Kibu Denis akifunga bao safi akimalizia krosi ya chinichini kutoka kwa Lary Bwalya.

Simba waliendelea kuliandama lango la wageni mnamo dakika ya 29 Mshambuliaji John Bocco aliwainua mashabiki wake akipachika bao la pili baada ya Lary Bwalya kupiga pasi safi.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 49 wakiwa na tofauti ya Pointi 8 na Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 57 wote wakiwa wamecheza mechi 23 na 7 kila mmoja huku Kagera Sugar wakishika nafasi ya saba wakiwa na Pointi 29.

Mchezo mwingine Coastal Union wameendelea kung’ara katika uwanja wao wa Mkwakwani jijini Tanga baada ya kuicha bao 1-0 Biashara United.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments