SIMBA SC YAINYUKA RUVU SHOOTING KWA MABAO 4-1


KLABU ya Simba imeinyuka Ruvu Shooting mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi ya NBC, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ambayo iliibua hisia za mashabiki wa klabu hiyo mara baada ya mastaa wao kucheza kandanda safi liliwafanya kufurahia kwenye dimba hilo.

Kibu Dennis alianza kuiandikia bao la kwanza timu yake katika kipindi cha kwanza na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0.

Kipindi cha pili Simba Sc iliendelea kulisakama lango la Ruvu Shooting na kufanikiwa kupata bao safi kabisa kutoka kwa kiungo mshambuliaji raia wa Zambia Larry Bwalya na kuiwezesha timu yake kuongoza kwa mabao 2-0.

Simba Sc iliendelea kutafuta mabao zaidi hivyo baadae Mshambuliaji ambaye hakuwa vizuri kabisa msimu huu John Bocco nae aliiandikia bao timu yake baada ya kupokea pasi bzuri kutoka kwa Yussuf Mhilu na baadae Henock kupachika bao la nne.

Bao la Ruvu Shooting la kufutia machozi lilifungwa na Haaruna Chanongo dakika ya 83 ya mchezo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments