SIMBA SC YALAZIMISHA SARE 1-1 MBELE YA GEITA GOLD CCM KIRUMBA MWANZA

Klabu ya Simba imeshindwa kufurukuta mbele ya Geita Gold Fc mara baada ya kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mcehzo huo ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirimba Mwanza.


George Mpole ameendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani mara baada ya leo kupachika bao kwenye mchezo huo na kuendelea kufukuziana na Fiston Mayele katika kinyang'anyiro cha mfungaji bora wa ligi.

Simba Sc imeilaisishia Yanga Sc katika mbio za ubingwa ambao mpaka sasa Yanga Sc inahitaji pointi 4 tu itangaze ubingwa kwenye ligi ya NBC.

Bao la Simba limewekwa kimyani na Kibu Dennis nae akiwa ana wakati mzuri katika mechi tano za hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments