SIMBA SC YALAZIMISHA SARE MBELE YA NAMUNGO FC

 


KLABU ya Simba Sc imelazimisha sare ya 2-2 dhidi ya timu ya Namungo Fc mchezo wa ligi ambao ulipigwa kwenye dimba la Ilulu Mkoani Lindi.

Namungo ilianza kupata bao kupitia kwa kiungo wao Jacob Masawe ambaye alipachika bao kali baada ya kupigwa kona na Shiza Kichuya na kumalizia nyavuni.

Simba Sc iliandelea kutafuta bao lavkusawazisha kwa kujaribu kutengeneza nafasi nyingi lakini baadae walibahatika kusawazisha bao kupitia kwa Shomari Kapombe.

Mechi mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-1 kabla ya Obrey Chirwa kuoachika bao la kuongoza kwa timu yake na baadae dakika za lala salama Simba Sc kusawazisha kupitia kwa Kibu Dennis.

Mchezaji wa Namungo Fc, Hashimu Manyanya alipewa kadi nyekundu mara baada ya kuoneshwa kadi za njani mbili kwa utovu wa nidhamu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments