TAASISI WEZESHI ZIONDOE UKIRITIMBA KWENYE MAENEO YA UWEKEZAJI-RC KUNENGE

Mkoa  wa Pwani umejipanga Kuwa ukanda wa Viwanda , Uwekezaji na mkoa wa kimkakati, Kutokana na Hilo Taasisi wezeshi za Serikali , Halmashauri zimeaswa kuondoa ukiritimba kwenye utoaji vibali na kutokuwa sehemu ya  kukwamisha juhudi za kukuza sekta ya uwekezaji.


Aidha Taasisi hizo ,zimeagizwa kuhakikisha zinafika katika maeneo ya Kongani za uwekezaji kutoa msaada pale inapotakiwa.

Akitembelea baadhi ya Kongani za uwekezaji wa Viwanda ikiwemo Kampuni ya SINOTAN (Kibaha Industrial Park Ltd ) , kujionea maandalizi ya miradi ,Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema hatokubali kuona Taasisi ambayo itaweka urasimu ili kudidimiza juhudi zinazofanywa na mkoa na Taifa kijumla.

Alifafanua, Eneo la Sinotan  lipo Kwala linatarajiwa Kuwa kubwa katika BARA LA AFRIKA ,lina ukubwa wa heka 2,500 na walishakabidhiwa miezi miwili iliyopita na litajengwa viwanda zaidi ya 200.

"Tunaona namna gani Rais Samia Suluhu Hassan anavyopambana kuinua sekta ya uwekezaji na kuitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji ,niahidi mkoa wa Pwani utakuwa nyuma yake kusimamia kongani hizi na kuboresha miundombinu ya uwekezaji"

Kunenge aliwakaribisha wawekezaji Duniani ,waje kuwekeza Mkoani hapo kwani Ni eneo salama kwa uwekezaji, Mazingira Bora na Ni mkoa wa kimkakati.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni nyingine ya Uwekezaji Yusuph Manzi alieleza , maandalizi yanakwenda vizuri ambapo awamu ya kwanza itamamilika mwezi wa kumi na baada ya hapo wataanza awamu ya pili .

Manzi alisema, matarajio yao ni kuwa eneo kubwa la uwekezaji ambalo litaleta tija kwenye Pato la Taifa na kuongeza ajira .

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri, alisema Kibaha imetenga maeneo ya uwekezaji na kwasasa wanahakikisha wanasimamia mipango ya Halmashauri na kuzisimamia Taasisi zote ili kuondoa vikwazo vitakavyorudisha nyuma juhudi za Serikali.

Licha ya mkoa huo kusheheni viwanda kila wilaya ,kwasasa Lina Jumla ya kongani 23 za uwekezaji ambazo zinazotarajia kuinua maendeleo na uchumi wa mkoa na Taifa na kupunguza mkali ya ukosaji wa ajira .





TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments