TIA SINGIDA WAHITIMISHA TAMASHA LA WIKI YA MICHEZO, WAHIMIZWA KUHAMASISHA SENSA

Mgeni Rasmi Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani (mwenye skafu) akimkabidhi kombe kepteni wa timu ya mpira wa miguu ya Diploma mwaka wa kwanza, Anuary Amimu (kushoto) baada ya kuibuka washindi dhidi ya Timu ya Bachelor mwaka wa pili katika Tamasha la Michezo la wiki moja la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida lililofikia tamati leo Mei 23, 2022 katika viwanja vya kampasi hiyo mjini Singida. Kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo, Mwalimu Ambwene Kajula na Muhadhiri Flora Lemnge. 
Furaha baada ya ushindi.
Mshindi wa MISS TIA, Haika Amiry (katikati) akiwa na mshindi wa pili Sumaiya Adam (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Tumaini Donald (kula) wakati wakiangalia fainali ya mpira wa miguu kati ya wanafunzi wa Diploma mwaka wa kwanza na Bachelor mwaka wa pili.
Furaha ya ushindi baada ya kukabidhiwa kombe kwa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza.
Majaji wa tamasha hilo wakijitambulisha kwa staili ya kusakata Rhumba.
Wanafunzi wakiwa kwenye tamasha hilo.
Tamasha likiendelea.
Bidhaa za Mjasiriamali Eddy  Ice Cream ambaye ni mwanafunzi wa TIA zikioneshwa kwenye tamasha hilo.
Mjasiriamali Eddy, akielezea jinsi alivyopata wazo la kuanzisha ujasiriamali huo akiwa shuleni ambapo alitoa wito kwa wanafunzi wenzake kuwa wabunifu na kuanzisha biashara yoyote au kufungua kampuni wakiwa masomoni kama alivyofanya.
Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dk.James Mrema akikabidhiwa bidhaa zinazotengenezwa na wanafunzi wajasiriamali wa taasisi hiyo.
Bidhaa zikikabidhiwa kwa wanafunzi.
Dk. Mrema akipokea bidhaa za wajasiriamali wanafunzi.
Viongozi wa taasisi hiyo wakipata viburudisho kwenye tamasha hilo.
Mmoja wa wagombea nafasi ya MISS TIA akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Taswira ya tamasha hilo.
Washiriki wa MISS TIA wakiwa jukwaani na vazi la ubunifu.
Madansa wakionesha umahiri wa kusaka dansi.
Warembo wakipita jukwaani.
Warembo wakiwa jukwaani na vazi la utamaduni.
Warembo wakiwa na vazi la ufukweni.
Mrembo akipita jukwaani na vazi la ofisini.
Warembo wakiwa na vazi la ofisini
Madansa wakionesha umahiri wakulitawala jukwaa huku mmoja wapo akiwa ameruka juu
Vazi la ufukweni hilo
Vazi la ufukweni hilo.
Mrembo akipita jukwaani.
Vazi la utanashati likioneshwa.
Vazi la ofisini likioneshwa.
Vazi la ofisini hilo.
Vazi la ufukweni hilo likioneshwa.
Tamasha likiendelea..
Mashindano yakiendelea. Mtanashati huyo akipita jukwaani.
Mshereheshaji (MC) akifanya yake jukwaani.
SIR.event Mwenzegule akifanya yake jukwaani.
Mrembo akipipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Mrembo akipita jukwaani
Picha zikipigwa kwenye tamasha hilo.
Tamasha likiendelea.
Tamasha likiendelea.
Majaji wakiwa kazini.
Vipaji vya mziki vikitafutwa.
Ngoma za Pwani zikipigwa nafikiri ni mdumange au Sengeli hilo.
Diana Happe akiwatoka wapinzani wake katika mchezo wa Netball.
Agnes Msigwa akionesha umahiri wa kudaka mpira katika mchezo huo.
Heka heka uwanjani zikiendelea.
Wanafunzi wakiwa uwanjani kuangalia kabumbu kati ya Timu ya Diploma mwaka wa kwanza dhidi ya Bachelor mwaka wa pili.
Tamasha likiendelea.
Wanafunzi wakiwa uwanjani. Ni bonge la Nyomi.
Joseph Dida wa Timu ya Bachelor mwaka wa pili akimtoka mchezaji wa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza Gadafi Omari.
Joseph Dida wa Timu ya Bachelor mwaka wa pili akimpigisha kwata mchezaji wa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza Gadafi Omari.
Kepteni wa Timu ya Diploma mwaka wa kwanza Omega Mwamkinga akichomoka na mpira dhidi ya mchezaji wa timu ya Bachelor mwaka wa kwanza. 
Tamasha likiendelea.
Washindi wakishangiliwa.
Mchezo dhidi ya Diploma mwaka wa kwanza na Bachelor mwaka wa pili  ukiendelea
Watizamaji wakiendelea kuangalia mchezo huo.
Ushangiliaji ukiendelea.
Mchezo ukiendelea.
Mchezo ukiendelea.
Mratibu wa Tamasha hilo, Mwalimu Ambwene Kajula akitoa neno la shukurani.
Zawadi ya mbuzi ikitolewa na mgeni rasmi.
Zawadi ya mbuzi ikitolewa.

Medani zikifikwa kwa washiriki wa tamasha hilo.

Watu na kombe lao nifuraa tupu kwa Timu ya Diploma.
Nifura tupu.
Mgeni rasmi akikabidhi ng'ombe kwa kepteni wa Timu ya Diploma.
Wachezaji wa timu ya Diploma wakiwa na ng'ombe wao.
Zawadi zikitolewa.
Zawadi zikitolewa kwa Ma Miss.
Mgeni rasmi akimvika Medani mratibu wa Tamasha hilo, Mwalimu Ambwene Kajula.Kulia ni WARDEN wa TIA, Asia Hansy.
Mgeni rasmi akitoa pongezi kwa washiriki wa tamasha hilo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Bachelor mwaka wa pili na viongozi mbalimbali wa TIA.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Diploma mwaka wa kwanza na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo..

Afisa Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani akimpongeza mjasiriamali mwenye kampuni ya Eddy Ice Cream ambaye ni mwanafunzi wa TIA alipotembelea duka lake. 

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imemaliza  rasmi wiki ya Tamasha la Michezo huku wakimihizwa kutumia michezo kuhamasha jamii kushiriki sensa ya watu na makazi itakayofanyika hapa nchini Agosti 23,2022.

Akifunga michezo hiyo Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mwaka huu tamasha hilo la michezo lilikuwa na mwamko mkubwa na kueleza michezo ni furaha, amani na ni ajira.

Alisema kijana yeyote ambaye hathamini kipaji chake atakuwa ni kijana ambaye hajitambui kwa kuwa kila kijana Mungu amempa kipaji chake kuna wachoraji, wacheza mpira, waimbaji hao wote ni karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu hivyo aliwaambia vijana hao waendelee kuvithamini vipaji vyao walivyonavyo.

Ndahani alisema matajiri wengi duniani sio kwamba wamesoma sana bali ni watu wenye vipaji hasa wasanii na wachezaji wa mpira ambao hata hapa nchini wapo.
"Mnapokuwa vyuoni endelee kuona namna gani mnaweza kuendeleza vipaji vyenu ili mfikie mafanikio" alisema Ndahani.

Ndahani alitumia nafasi hiyo kuwaomba vijana hao na wanamichezo wote kwa ujumla kutumia michezo kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la senza ya watu na makazi ambalo litafanyika Agosti 23 mwaka huu.

Mratibu wa tamasha hilo  Mwalimu Ambwene Kajula alisema michezo iliyofanywa katika tamasha hilo ni mpira wa pete, mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, mchezo wa bao na kuinua vipaji kwa kutafuta MISS na MR tia, waimbaji, wachekeshaji, waigizaji, wacheza muziki na ngoma, watanashati, wabunifu, wasiriamali.  

Pia alisema washiriki wa shindano la MISS TIA waliweza kupita jukwaani wakiwa wamevaa vazi la ufukweni, ubunifu, utamaduni na ofisini huku MR TIA wakivaa vazi la ufukweni, utamaduni na ofisini.

Alisema kuwa vilevile kulikuwa na maonyesho ya wajasiriamali mbalimbali wa ndani na nje ya Taasisi na kuwa kwao  ilikuwa ni fursa kubwa kwa wanafunzi wao na jamii nzima inayowauzunguka ambapo wametoa zawadi  kwa washindi mbalimbali akiwepo ng'ombe kwa mshindi namba moja , mbuzi,fedha taslimu na kufikwa medani kwa baadhi  ya washiriki.

Alitaja zawadi zilizotolewa kwa mshindi wa kwanza kwa mpira wa miguu ambao walikuwa ni wanafunzi wa diploma mwaka wa kwanza kuwa ni kombe na ng'ombe mmoja, mshindi wa pili wanafunzi wa Bachelor mwaka wa pili wao walipata mbuzi watatu, na wanafunzi wa Bachelor mwaka wa tatu ambao walikuwa washindi wa tatu wakiambulia zawadi ya mbuzi wawili.

Alisema kwa upande wa Netball wanafunzi wa diploma mwaka wa pili waliopata nafasi ya kwanza walipatiwa mbuzi watatu huku diploma mwaka wa kwanza waliokuwa washindi wa pili wakiambulia mbuzi wawili na mshindi wa tatu akipata cheti.

Alisema katika mchezo wa Basketball mshindi wa kwanza alipata mbuzi wawili na mshindi wa pili akiambulia mbuzi mmoja na halikadharika katika mchezo wa Volleyball zawadi zilikuwa hivyo hivyo.

Kajula alitumia nafasi hiyo kuipongeza TIA kwa kuweka wiki hiyo ya Tamasha la Michezo na hasa wanafunzi walioshiriki na wadau mbalimbali waliofanikisha kwa namna moja hama nyingine kufanyika kama Hoteli ya Jalmini na Cocacola kwani limewaongezea wanafunzi wao uelewa wa maisha na kwamba si elimu tu inayoweza kukufanikisha katika maisha ni wazi kazi na dawa ndio njia pekee ya mafanikio. 

Alisema kusoma kunahitaji uweze kucheza ili uweze kuelewa na si kucheza pekee ila kujishughulisha na shughuli zingine ili kutanua ubongo, kulinda na afya ya kiakili ili kutia chachu katika kupambana mawazo hasi na kuruhusu kuwaza katika mlengo chanya. 

Pia alisema michezo ni kukuza ushirikiano na urafiki kwani michezo hunoga pale mnapokuwa wengi na kujumuika kwa pamoja, Hii inamaana kwamba kidole kimoja hakivunji Chawa. 

Alisema michezo huwalinda wao na wengine waliokaribu nao kiafya, kiakili, kimwili na kuwa michezo inaweza kutumika kama njia bora sana katika kujikinga na maradhi mbalimbali na kuokoa kipato kinachoweza kutumika katika ununuzi wa madawa ya kujitibu na zaidi ya yote ni lazima wajikite katika kukuza vipaji vya wanafunzi.

"Tunapenda kuishukuru nchi yetu kwani toka enzi za mababu imekuwa ikijitahidi kuhakikisha wananchi wanajihusisha na michezo kwani hii husaidia katika ulinzi na usalama, kuzuia kutenda uhalifu, kuongeza ajira, kupunguza matumizi ya changamoto za kiafya nakadhalika hakika uhuru huu tulionao ndio pekee unaoturuhusu kupata nafasi ya kuweza kujikita katika shughuli hizi za maendeleo na tunaipongeza Serikali hii kwa dhati kwani Amani, Utulivu, iliyopo ni fahari kubwa sana kwetu na vizazi vyetu' alisema Mrema. 

Aidha Kajula alisema katika wiki hii ya michezo TIA kwa mwaka 2022 wanajivunia furaha waliyonayo japo kuwa kuna mambo kadhaa ambayo wanayatamani kama kuweka viwanja vya michezo vya kisasa ambavyo vitaamsha hari za wengi kujihusisha na michezo,kuweka uzio kuzunguka Taasisi hiyo ili kulinda maeneo yao na wanafunzi kwa ujumla katika changamoto mbalimbali wanazozipitia, kuongeza mabweni ya kisasa katika iddi kubwa ambayo itaweza kuwasaidia wanafunzi kujiingiza katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa wanakaa mtaani, kuwakinga wanafunzi katika maambukizi mapya ya magonjwa ya zinaa na VVU na UKIMWI.

Alitaja mambo mengine wanayoyatamani kuwa ni kuwakinga wanafunzi katika kujiingiza katika madawa ya kulevya na tabia hatarishi, kutumia mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na wadau wengine kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi ambao hawana uwezo kuweza kusomeshwa na kujikwamua katika janga la umaskini, kuwasaidia wanafunzi kupata ajira mbalimbali za muda mfupi na mrefu ili kuweza kupata fursa wakipambana na maisha.

Akizungumzia namna ya kujiunga na masomo katika chuo hicho kwa Mwanafunzi mwenye ufaulu kuanzia alama D4 anaweza kutuma maombi yake kwani atakuwa amekidhi sifa za kujiunga na dirisha liko wazi tangu Mei 14 hadi 15 Agost 2022. 

Alisema wanawakaribisha kujiunga na programu za fani ya Uhasibu na Fedha, Uhasibu wa Umma, Ugavi na manunuzi, usimamizi rasilimali watu, masoko na uhusiano wa umma, usimamizi wa biashara. Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti  ya tassisi yaani www.tai.ac.tz au wanaweza kufika chuoni na kujaza fomu hizo. Pia wanaweza kupata fomu hizo katika shuile za sekondari walikohitimu kidato cha nne na kuwa wanawahakikishia kuwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania inatoa elimu bora yenye ujuzi wa maarifa na vitendo hivyo kumjengea mhitimu weledi na uwezo mkubwa wa kujiajiri na kuajiriwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments