Tozo Daraja La Nyerere Zashuka, Kulipwa Kwa Vifurushi

Hatimaye Serikali imesikia kilio cha wananchi juu ya malipo ya kuvuka daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Saalam na kubadili mfumo wa malipo ambao unaelezwa utakuwa na ahueni.

Watumiaji wa daraja hilo sasa wataweza kufanya malipo ya siku (mara moja) bila kujali watapita mara ngapi wakati malipo ya wiki na mwezi yakisubiri kukamilika kwa marekebisho ya mifumo.

Hata hivyo Mbunge wa jimbo hilo, Dk Faustine Ndugulile alisema kilio cha wakazi wa Kigamboni ni tozo hizo kuondolewa kabisa.
“Kuanzia sasa baadhi ya tozo zitakuwa zitakazokuwa zinatozwa ni ile ya bodaboda bei itakuwa Sh300 kwa safari, Sh500 kwa siku, Sh2, 000 kwa wiki na Sh5, 000 kwa mwezi,” ameeleza Dk Ndugulile.

Awali bodaboda katika eneo hilo zilikuwa zikilipia Sh600 kila zilipopita jambo ambalo lilikuwa likilalamikiwa.

Bajaji sasa zitalipa Sh500 kwa safari, Sh3,000 kwa siku, Sh10,000 kwa wiki na Sh20,000 kwa mwezi hii ni kutoka Sh1,500 iliyokuwa ikilipishwa awali kwa kila safari kwa baiskeli za miguu mitatu yaani guta, mikokoteni na bajaji.

Magari madogo sasa yanalipia Sh1,500 kwa safari, Sh2,500 kwa siku, Sh12,000 kwa Wiki na Sh35,000 kwa mwezi ikilinganishwa na Sh1,500 iliyokuwa inatozwa kwa kila safari katika daraja hilo.

Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa uwekezaji kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Gabrieli Silayo alisema tayari wamepokea maelekezo kutoka wizarani juu ya mpango huo na kwamba wanaanza taratibu za kubadilisha mifumo ili kuendana na mabadiliko hayo.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments