Recent-Post

Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Mei 6, 2022

 LEO Dola ya Zimbabwe (ZWD) inanunuliwa kwa shilingi 0.43 na kuuzwa kwa shilingi 0.44 huku Shilingi ya Uganda (UGX) ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Muonekano wa noti za shilingi 2000 za Tanzania.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 6,2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Aidha, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.7 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2416.4 na kuuzwa kwa shilingi 2441.5.
Kwa mujibu wa BoT, Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Franka ya Rwanda (RWF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.

Aidha, Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.6 na kuuzwa kwa shilingi 2310.5 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 145.91 na kuuzwa kwa shilingi 147.26.
Kwa upande wa Kwacha ya Zambia (ZMK) inanunuliwa kwa shilingi 133.4 na kuuzwa kwa shilingi 135.7 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.07 na kuuzwa kwa shilingi 50.52
NA GODFREY NNKO

Post a Comment

0 Comments