Waandishi Mikoa Saba Kunufaika Na Mafunzo Ya Ulinzi Na Usalama.

Muungano wa Klabu za  Waandishi wa Habari nchini (UTPC) kwa  kushirikiana Shirika la Kimataifa la Kusaidia Vyombo vya Habari(IMS) wameanza kutoa mafunzo ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa mikoa saba nchini.

Akizungumza katika mjadala kuelekea maadhimisho ya siku ya vyombo vya habari Duniani leo Mei 2, Mratibu wa UTPC Victor Maleko amesema lengo la mradi huo ni kuwawezesha wanahabari kufanyakazi vizuri na kwa usalama zaidi.

Maleko amesema katika mradi huo, waandishi wa habari watapewa elimu katika matumizi sahihi yamitandao, lakini pia kuweza kuchukuwa tahadhari za kiusalama.
Ametaja mikoa hiyo ni Arusha, Shinyanga, Mwanza, Morogoro, Kigoma, Dodoma na Zanzibar.

Mradi huu unakwenda sambamba na kuandaliwa mijadala kuhusu usalama katika utendaji kazi kwa kushirikisha vyombo vya dola," amesema.
Akizumgumzia mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa UTPC, Abubakar Karsani amesemamradi huo ambao tayari umeanza katika maeneo kadhaa na umeanza kuonesha manufaa makubwa
Waandishi wa habari zaidi ya 350 kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na wadau wa habari, wanakutana jijini Arusha, katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani ambayo yanaendelea jijini Arusha.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments