Waandishi wa habari waaswa matumizi ya sahihi mitandao


 Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwa na matumizi sahihi ya habari wanazotoa katika mitandao ya kijamia ili kuonesha tofauti yao na wasio na taaluma ya habari.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Gerson Msigwa ametoa wito huo leo Jumapili Mei Mosi 2022 katika warsha kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo Habari Duniani (WPFD) ambayo kitaifa inafanyika jijini Arusha.

Amesema katika maadhimisho hayo ambayo kauli mbiu yake ni vyombo vya habari na changamoto za kidijitali ni muhimu kuzingatia sheria katika matumizi ya mitandao.

Amesema Serikali imesajili runinga za mitandao karibu 500 lakini ni muhimu kuwa na maudhui bora ambayo yanaweza kutofautiana mwanahabari na asiye mwanahabari.

Amesema pia muhimu kuzingatia sheria na maadili kwani tayari imewahi kutokea baadhi ya wanahabari kutumia vibaya uhuru wao.

"Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kisikia malalamiko kutoka kwa wadau alitoa maelezo tuzungumze na tayari Waziri wa Habari Nape Nnauye ameanza mazungumzo na wadau" amesema

Msigwa amesema hivi sasa wadau wa habari wanafursa ya kupeleka serikalini hoja zao kwa maeneo ambayo wanadhani yanamapungufu na watakaa pamoja kujadiliana na ambayo yanaonekana yanahitaji maboresho yatafanyika.

"Ambayo hayawezekani tutakaa na wadau na tutatoa sababu moja mbili tatu na tutafikia muafaka kwa sababu kuna jambo wewe unaweza kuona halifai mwingine akasema linafa sasa hatujuwahi kufunga milango kupokea maoni" amesema

Awali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Babile amesema mazingira ya vyombo vya habari na wanahabari kufanya kazi nchini yanaendelea kuboreshwa na Serikali tofauti na miaka michache iliyopita.

Babile amesema tayari wameanza majadiliana na Serikali juu ya maboresho ya Sheria kadhaa ambazo zinaminya uhuru wa habari nchini.

Akizungumza katika Warsha hiyo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA- Tan) Salome Kitomari amesema kuna haja ya kuendelea kuboreshwa Sheria mbalimbali za habari sio Tanzania pekee bali nchi kadhaa za kiafrika.

Amesema nchi kadhaa zimekuwa zikitunga Sheria ambazo zinafanana akitolea mfano wakati wa chaguzi matumizi ya mitandao yamekuwa yakidhibitiwa katika nchi kadhaa jambo ambalo sio sahihi.

Kitomari amesema wanahabari wanaadhimisha siku ya uhuru wa habari bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwepo maslahi duni hivyo muhimu kuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu kukabiliana na changamoto hii.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments