WAFANYAKAZI KUTOTIMIZIWA STAHIKI ZAO KUNAWAPUNGIZIA ARI YA KUFANYA KAZI KWA JUHUDI:TUCTA SINGIDA

 

 Mkuu wa Mkoa  Singida Dk. Binilith Mahenge akihutubia Wafanyakazi katika Sherehe za  Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi iliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Namfua (Liti), Manispaa ya Singida jana.

Wafanyakazi wakiwasili uwanjani wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali na kuonesha idara wanazotoka ikiwa ni kusheherekea kilele cha maadhimisho ya sikukuu hiyo.

Mkuu wa Mkoa Dk.Binilith Mahenge akiwa na viongozi wengine wakipokea maandamano hayo.
Viongozi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Maandamano yakiwasili kwenye uwanja huo.


Maandamano yakipita mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa Dk.Binilith Mahenge (kushoto) akiwa na viongozi wengine wakipokea maandamano hayo.
Sherehe  zikiendelea.
Wafanyakazi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Magari yaaaaaa maandamano yakipita mbele ya jukwaa kuu.

 Wafanyakazi wakiimba wimbo wa Mshikamano ktika kilele cha maadhimisho ya sikukuu hiyo.

Wimbo wa mshikamano ukiimbwa.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Mratibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Singida, Susan Shesha ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Dk.binilith Mahenge katika sherehe hizo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akizungumza kwenye sherehe hizo.
Wanakwaya wa Chuo cha Utumishi wa Umma Singida wakitoa burudani.
Burudani ikiendeleaa.
Mratibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Singida, Susan Shesha ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida akikabidhi risala kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Dk.binilith Mahenge.
Msanii Mussa Mashairi (kushoto) akiupiga mwingi kwenye sherehe hiyo

  Kikundi cha ngoma za utamaduni cha Mbalamwezi cha Manispaa ya Singida kikitoa burudani katika sherehe hizo.

Mshereheshaji wa sherehe hiyo (MC) Salma Mwijuma akiwajibika.
Mratibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Singida, Susan Shesha ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida (kulia) akiongoza kucheza kwaito kwenye sherehe hizo.
Kwaito likiendelea.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos akizungumza wakati akitoa salamu kwenye sherehe hizo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Ester Chaula akizungumza wakati akitoa salamu kwenye sherehe hizo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akizungumza wakati akitoa salamu kwenye sherehe hizo.
MC Shikizi wa sherehe hizo (MC) Ibrahimu Mrua akifanya yake kwenye hafla hiyo

Mwakilishi wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Diwani wa Kata ya Mughanga, Vallerian Kimambo. akizungumza wakati akitoa salamu za manispa hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Melkzedeki Humbe akizungumza wakati akitoa salamu kwenye sherehe hizo.

Sherehe zikiendelea.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, John Mgalula akizungumza wakati akitoa salamu kwenye sherehe hizo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matobora, akizungumza wakati akitoa salamu kwenye sherehe hizo.
Mwenyekiti wa dini mbalimbali Mkoa wa Singida, Hamisi Kisuke akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida akizungumza kwa niaba ya chama hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza kwenye sherehe hizo wakati akitoa salamu za wilaya hiyo.

Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Hamisi Mtundua akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wafanyakazi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wenzake baada ya kukabidhiwa zawadi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, John Mgalula akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wenzake baada ya kukabidhiwa zawadi.
Utoaji zawadi ukiendelea.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Kulwa Juma Mzumya akikabidhiwa zawadi ya mfanyakazi bora.
 

SHIRIKISHO la vyama vya Wanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Singida limesema kutowatimizia wafanyakazi stahiki zao kunawasababishia kukosa ari ya kufanyakazi  kwa     juhudi.

Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Singida, Susan Shesha ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Singida wakati akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Dk.binilith Mahenge katika maadhimisho ya sherehe ya wafanyakazi duniani iliyofanyika jana kimkoa Uwanja wa Namfua (Liti) 

"Nitaje baadhi ya mambo hayo yanayofifisha ari ya wafanyakazi kushindwa kufanya kazi kwa juhudi kuwa ni kutopata nyongeza ya mshahara kwa muda mrefu, shirika la bima kutowalipa watumishi waliokata bima ya maisha  pindi bima zao zinapoiva hivyo kupelekea malalamiko mengi kwa watumishi waliojiunga na bima hiyo" alisema Shesha.

Alitaja mambo mengine kuwa ni madai ya fedha za uhamisho, likizo pamoja na malimbikizo ya mishahara kucheleweshwa hadi wengine kustaafu, baadhi ya wakurugenzi kutohuisha mabaraza ya wafanyakazi kwa wakati, waajiri wengi wa sekta binafsi kutojua sheria ya ajira na mahusiano kazini, sheria ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi na sheria ya usalama mahala pa kazi na waajiri binafsi kutowasilisha makato ya asilimia 10 kwenye mfuko wa Hifadhi ya Jamii changamoto ambayo uwakumba wafanyakazi wa sekta binafsi na kuwafanya wasione umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Shesha aliendelea kutaja sababu zingine kuwa ni bima ya afya  kuchagua baadhi ya dawa kulipia kwa makato ya bima, kutoundwa kwa bodi ya kima cha chini cha mshaahara,kutotolewa kwa huduma ya afya kwa wanachama  wastaafu kutoka mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa kwa sekta binafsi, kutohimitishiwa kikamilifu zoezi la watumishi wa umma wa darasa la saba waliositishiwa ajira zao, makato ya ya bodi ya mikopo ya Elimu ya juu yazingatie mikataba ya wanufaika na waajiri kutopeleka michango ya hifadhi ya jamii kwa wakati hivyo kupelekea tozo kubwa na kusababisha wastaafu kuchelewa kupata pensheni zao.

Katika risala hiyo watumishi hao walitoa baadhi ya maombi yao kwa serikali kuwa nyongeza ya mishahara iendane na hali ya uchumi wa sasa, uhamisho wa watumishi uendane na ulipwaji wa stahiki zao kwani kuendelea kuhamisha bila malipo kunapingana na taratibu za utumishi na wanaiomba Serikali ilipe madeni ya watumishi kwa wakati ili kurejesha imani ya watumishi kwa Serikali yao.

Mambo mengine walioomba ni waajiri wa sekta binafsi watoe mikata mikataba ya kudumu kwa wafanyakazi, likizo na kima cha chini cha mshahara kizingatiwe, mabaraza ya kazi yafanyike kwa wakati na malipo ya posho yatolewe kwa mujibu wa sheria na isiwe hisani ya mwajiri, wafanyakazi wanaolipwa kwa mapato ya ndani (GF) walipwe mishahara yao kwa wakati na malipo ya wastaafu yalipwe kwa wakati.

Shesha alisema maombi yao mengine ni kodi kwenye mishahara iendelee kupunguzwa, baadhi ya waajiri, viongozi wa serikali na kisiasa wenye tabia ya kuwaadhibu watumishi bila kuzingatia sheria na kanuni za utumishi kuacha kufanya hivyo ambapo walimuomba mkuu wa mkoa  ofisi yake itilie mkazo kwa wajiri ambao hawataki kuchangia katika sherehe za Wafanyakazi Mei Mosi.

Akizungumzia mafanikio waliyopata ni waajiri kutoa fursa kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutimiza majukumu yao bila kubughudhiwa, ushirikiano mzuri wa vyama hivyo na waajiri hasa wakurugenzi wa katika halmashauri, kuendelea kuwa na amani katika nchi kumezidi kuchochea ufanisi kazini kwa sababu wafanyakazi hufanya kazi bila hofu.

Aidha Shesha alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kwa kuwapandisha madaraja watumishi na ulipwaji wa malimbikizo yao waliyokuwa wakidai.

Dk. Mahenge akizungumza baada ya kupokea risala hiyo alisema mambo yote yaliyondani ya uwezo wake atayafanyia kazi na yale ya kitaifa yatapelekwa kwa wahusika ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuiletea nchi maendeleo.

Alisema Serikali imefanya kazi kubwa mno ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo kwa mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Singida ulipewa Sh.232 Bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa mirad imbalimbali.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko aliwaambia wafanyakazi hao kuwa baada ya sherehe hiyo waende wakafanye kazi kwa bidii na kwa ' step' kama walivyokuwa wakicheza vizuri kwaito na si vinginevyo.

Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Hamisi Mtundua akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wafanyakazi alishukuru Serikali kwa kazi kubwa iliyoifanya mkoani hapa ya miradi mbalimbali kama ujenzi wa vituo vya afya, miradi ya maji, ujenzi wa madarasa, ujenzi wa zahanati, barabara na umeme.

Alimpongeza Mkuu wa Mkoa Dk. Binilith Mahenge kwa kazi nzuri anayoifanya mkoani hapa na kusimamia utelekezaji wa miradi hiyo kwa uaminifu mkubwa kwa kushirikiana na watendaji wake wakiwemo wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa wilaya na watumishi wa kada mbalimbali.

Katika sherhe hizo watumishi waliofanya vizuri walitunukiwa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu na Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ilitangazwa kuwa ya kwanza kwa kuongeza fedha za zawadi kutoka Sh.300,000 hadi Sh.500,000 huku Wilaya ya Itigi ikiibuka mshindi kwa kushika nafasi ya kwanza ikifuatia Ikungi kwa kuwajali watumishi na ushirikiano mkubwa wanaovipa vyama vya wafanyakazi mkoani hapa na kuwa halmashauri bora ambazo hazina malamiko makubwa ya watumishi kwa kuwatendea haki.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments