Wafugaji Wamjeruhi Mwenzao Kwa Mishale Igunga

Mfugaji Masalago Manyenye Gamuga (30) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Isakamaliwa Wilaya Igunga amenusurika kuuawa baada ya kushambuliwa kwa fimbo na mishale na watu wanane wanaodaiwa kuwa nao ni wafugaji.

Akizungumza na Mwananchi akiwa amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Igunga, Gamuga amesema kuwa watu hao wamemshambulia jana.

Amesema akiwa anachunga mifugo yake ghafla watu wanane wakiwa na fimbo na mishale walimsalimia kisha kuanza kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Ameongeza kuwa baada ya kuona hali hiyo alianza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo aliwasikia watu hao wakisema acheni kumpiga na fimbo tumieni mishale ndipo akachomwa mishale miwili.

Watu hao walimchoma Gamuga mshale mmoja shingoni na mwingine kwenye ubavu wa kushoto.

“Mimi sijui kama nitapona kwani watu hao wamenijeruhi vibaya sana wamenipiga mshale kwenye mbavu ya kushoto na mshale mwingine kwenye shingo hata hivyo hawakuishia hapo mwingine alinichoma kisu kwenye tumbo nikishuhudia mwenyewe”, amesema

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo akisema chanzo ni kutofautiana wachungaji kuhusu malisho.


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments