WAKAZI WILAYA YA MANYONI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANATUNZA CHAKULA KUJIHAMI NA UHABA WACHAKULA

Wakazi wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida,wametakiwa  kuhakikisha wanatunza chakula kilichopo, ili kujihami na uhaba wa chakula ambao unaweza kutokea hapo baadae.

Wito huo umetolewa juzi na naibu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Manyoni, Fadhki Chimsala,wakati akifungua warsa ya siku moja, iliyohusu kutathimini na kutatua changamoto za ufugaji wa mifugo. Na masuala ya kilimo na mazingira vijijini.

Anasema kuwa hali ya hewa msimu huu,haikuwa nzuri hivyo kuna kila dalili kuwa kutakuwepo na upungufu wa chakula.

“Kwa hiyo naomba niwasihi wananchi,wahakikishe wanatumia chakula vizuri na wawe na akiba itakayokidhi mahitaji ya mwaka mzima.Nawatahadharisha wananchi wasishawishike  na fedha za wafanyabiashara,wakauza nafaka”,alisema Chimsala ambaye ni afisa kilimo na mifungo wa halmashauri ya Manyoni.

Katika hatua nyingine,Chimsala,amesema halmashauri hiyo ina mpango wa kutenga maeneo ya malisho. Na wataelimisha wafugaji wapunguze mifugo, wabaki na ile itakayopata malisho ya kutosha .

Kuhusu warsha hiyo,naibu mkurugenzi huyo,amewataka waalikwa watumie vema fursa hiyo,kwa kuchangia, ili waweze kutoka na mikakati/mkakati itakayopelekea kuwa na ufugaji mifugo wenye tija.

Naye afisa kilimo na mifugo mkoa wa Singida,Dk.David Mruma,amewaagiza wakazi mkoani hapa,wasiruhusu wafugaji kuhamia kwenye maeneo yao bila kuwa na kibali halali.

“Mfugaji anayehamia hakikisheni anakuwa na kibali kilichotolewa na uongozi anakohamia.Pia awe na kibali kingine kutoka huko anakohama.Hii ni kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu”,alisema Dk.Mruma.

Dk.Mruma amezitaka halmashauri ziwe makini kwa madai kuna baadhi ya wafugaji,huhamisha mifugo yao usiku, na wengi wao wanakuaga hawana vibali.

Aidha,anasema mfugaji anayepata kibali halali cha kuhama,ahakikishe anasafirisha mifugo yake kwa gari au magari kama ana mifugo mingi.Lengo ni kuepukana na athari ya kupata athari ya mmomonyoko wa ardhi.

Afisa maliasili mkoa wa Singida,Charles Kidua,amesisitiza kwamba  kuna umuhimu mkubwa kuielemisha jamii/wafugaji, waondokene na ufugaji wa mifugo mingi.Kwa madai kuwa haina tija.

“Ufugaji wa mifugo mingi hauna tija, mbali ina changamoto nyingi ikiwemo kutokuwepo kwa malisho ya kukidhi mahitaji”,amesema afisa huyo.

Warsa hiyo,iliyosimamiwa vyema na afisa maliasili mkoa Kidua,wajumbe waliweka maazimo,kuwa ni pamoja na kufufua/kuanzisha majosho,kuchimba mabwawa,matumizi ya mbegu bora za nyasi na kutunza na kulinda mazingira.

Ilihudhuriwa na afisa kulimo na ufugaji mkoa,wilaya na kata,afisa mazingira mkoa,wenyeviti wa vijiji,wakulima na wafugaji.

Na iliandaliwa na kwa ushirikiano baina ya mashirika ya Helvetas Swiss Intercooperation,makampuni ya pamba ya Alliance na BioSustain na Jukwaa la kilimo Hai Tanzania (TOAM).


.Afisa kilimo na mifugo,Dk.David Mruma,akitoa mada yake kwenye warsha ya kutathimini na kutatua changamoto za ufugaji wa mifugo na masuala ya kilimo kwa ujumla.Washara hiyo,ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya Manyoni.

.Baadhi ya wajumbe waliohudhuria warsha ya kutathimini na kutatua changamoto za ufugaji wa mifugo na masuala ya kilimo kwa ujumla.Washara hiyo,ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano halmashauri ya wilaya Manyoni.Picha na Nathaniel Limu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments