Waliokosa Vyeti Vya Kidato Cha Nne Waendelea Kupiganiwa


 Sakata la watumishi wa umma walioondolewa kazini kutokana na ukosefu wa vyeti vya kidato cha nne, sasa limetua tena bungeni.

Leo Alhamisi Mei 19, 2022 Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani ameuliza kuhusu watumishi hao walioondolewa kwa kigezo cha kutokuwa na cheti cha kidato cha nne.

Mbunge huyo amehoji nini kauli ya Serikali ili waliokuwa watumishi hao waweze kuapata haki yao.

Akijibu swali hilo bungeni, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema jambo hilo linaendelea kufanyiwa kazi na mamlaka mbalimbali na utekelezaji wake upo mbioni.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeshaunda tume ya kufuatilia jambo hilo kutokana na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alitoa msamaha kwa kundi hilo na kutaka watazamwe na ikibidi walipwe asilimia tano ya pensheni zao.

“Kwa huruma yake Rais aliagiza kuunda tume ili tuweze kuwapitia waliokuwa watumishi ili walipwe asilimia tano ya pensheni kwenye michango waliyokuwa wanachangia, hivyo tuache kwanza tume ipitie tutakuwa na majibu sahihi,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ametaka kundi hilo kuwa na uvumilivu ili kazi ya kuhakiki iweze kufanyika na kupeleka haki kwa wanaostahili kuipata haki hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments