WALIOPATIWA FEDHA ZA TASAF WILAYANI LINDI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUGUSA MAISHA YAO MOJA KWA MOJA

Uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza na Rais Samia Suluhu Hassan wa kuendelea kusaidia kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), umepongezwa na wananchi wa Mkoa wa Lindi ambao wamekiri uwepo wa mfuko huo umesaidia kugusa maisha yao moja kwa moja.


Wakizungumza mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ambaye alitembelea mradi wa upandaji miti ya minazi na mikorosho kwenye eneo hilo wananchi hao wamesema wanamshukuru Rais Samia kwa jitihada zake za kusaidia wananchi wa kipato cha chini kupitia mfuko huo.

Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzake wa Kijiji hicho, ambao wanajihusisha na mradi wa kilimo Cha mazao mbalimbali ya biashara ikiwemo minazi, Dalini Makwaya, amesema kupitia fedha hizo wameendelea kuimarika kiuchumi kwa kujijihusisha na miradi ya maendeleo.

"Tunamshukuru Serikali ya Rais Samia kwa kwa mpango huu kwa kuwa umetusaidia sisi kaya masikini, kupitia fedha hizo tumekata bima za afya, tunanunua sare za wanafunzi wetu na kubwa zaidi tunanunua chakula, kwa hili tunasema Asante Rais wetu," amesema Makwaya.

Kwa upande wake Shaka ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani Lindi amesema amefurahishwa kusikia wananchi wenyewe wanakiri na kuwa mashuhuda walivyonufika na mpango wa Serikali wa kusaidia kaya masikini kupitia mfuko wa TASAF.

Shaka amefafanua Rais Samia anayodhamira ya dhati kuwaondoa wananchi wa maeneo mbalimbali kwenye lindi la umasikini na ndio maana amekuwa na uthubutu wa kuzungumza magumu yote badala ya kuyafunika funika akaonyesha ama kuwapa matumaini wananchi wake ambayo tunaweza tukafika lakini tunaweza tukachekewa.

"Rais amekuwa muwazi kabisa na ndio maana mkuu wa Mkoa wa Lindi kupitia 'statment' (maelezo) kwamba Rais ameamua kwa makusudi kuweka nguvu kwenye mkoa huu ili kuleta mabadiliko, kwanza ya huduma za kijanii pamoja na kuleta mabadiliko katika huduma hizi za kiuchumi," amesema Shaka.

Akielezea zaidi amesema wananchi wamekiri kwamba kwa miaka mingi Mkoa wa Lindi ulikuwa ukipata fedha kidogo lakini tangu Rais Samia aingie madarakani mkoa huo umeendelea kupata fedha nyingi ambazo zinatumika kutekeleza miradi ya maendeleo.

"Nishukuru na kuwapongeza TASAF kwa kuleta fedha hii moja kwa moja kwa wananchi. Nimeona kupitia program yenu kwa siku mwananchi mmoja ananufaika na fedha kwa kiasi gani kwa mwezi, ni fedha nyingi kidogo," amesema na kusisitiza kuwa kinachofanywa na Rais Samia ni kutekeleza ailani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

"Niwaahidi Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia itaendelea kuguswa na shida za wananchi kupitia utekelezaji wa Ilani ya Chama chetu. Na kwenye hili nataka niwatie nguvu kazi mnayoifanya ni nzuri katika mradi huu wa upandaji wa minazi ambayo katika kipindi hiki imeanza kupotea," anasema.

Wakati huo huo wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Tarek ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina hatua ambazo zinachukuliwa na Serikali ya mkoa katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba Rais Samia ametoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo.

"Hapa tulipo tumeona wananchi ambavyo wameendelea kuhamasika kufanya shughuli za uzalishaji mali, wameamua kupanda minazi na tunaamini baada ya miaka mitano wataanza kuvuna nazi na kujiingizia kipato.Kupitia fedha hizi za TASAF wananchi wameendelea kujiimarisha kufanya maendeleo kwa kubuni miradi yenye tija.

“Pia tuna tuna zao la korosho ambalo ni zao linauzwa kibiashara duniani na ushahidi ukifika msimu wa korosho wafanyabiashara kote duniani wanakuja mkoani Lindi kununua korosho.Kwaio tulichokifanya tunaendelea kuwahamasisha wananchi wetu hawa wanaopata fedha za TASAF waingie kwenye kilimo hiki.

“Kwasababu ukishaotesha mti na mti huo ukaota unauhakika kabisa kwamba miaka yako yote ya maisha yako ukienda ukifuata taratibu za kilimo unauhakika wa kuvuna.Nitumie nafasi hii kumshukiru sana Rais wetu kwa kujali kaya masikini kwa sababu anaendelea kutoa fedha na sisi kama Mkoa tunasimamaia kuhakikisha kaya zinazopata fedha hizi ni zile zinauhitaji wa fedha hizi,”amesema

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akipata maelezo kutoka kwa Dalini Makwaya kuhusu mche wa mnazi uliomo kwenye mradi wa kilimo cha minazi uliowezeshwa na fedha za mradi wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF) katika Kijiji Cha Kilangala, Manipaa ya Lindi mkoani Lindi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akishiriki ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Wialaya Lindi alipotembelea kukagua ujenzi wake akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akiwasha rasmi mtambo wa maji katika mradi wa maji wa Mitwelo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 Mkoa wa Lindi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Tarek kuinua tofali wakishiriki ujenzi wa Shule Maalumu ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi, alipotembelea kukagua ujenzi wa shule hiyo katika Kijiji Cha Kilangalala Manispaa na Mkoa wa Lindi.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akipata maelezo ya ujenzi wa Shule Maalumu ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Lindi, kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri Manispaa ya Lindi, Stahsin Mrema, alipotembelea kukagua ujenzi wa shule hiyo katika Kijiji Cha Kilangalala Manispaa na Mkoa wa Lindi. (Picha zote na Fahad Siraji wa UVCCM).

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wana CCM wakati alipotembelea Shina Namba 10 katika Kata ya Kilangala, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi mkoani Lindi, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Uhai wa Chama.

(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI WA CCM)

Post a Comment

0 Comments