WAPANDA BASKELI 30 WADHAMIRIA KUFIKA KILELE CHA MLIMA MERU

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, timu ya waendesha baiskeli wapatao 30 wanapanda mlima Meru ambao ni wa pili kwa urefu nchini.

“Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa baiskeli kufika katika kilele cha mlima meru,” Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi anayesimamia Uhifadhi na Maendeleo ya biashara, wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Bakari Mnaya, alibainisha.

Mlima Meru una urefu wa Mita 4566 kutoka usawa wa bahari. Ni wa pili kwa urefu nchini baada ya Kilimanjaro.

Katika kuweka rekodi hiyo mpya katika sekta ya utalii, hifadhi ya Taifa ya Arusha (TANAPA) imezindua utalii huu mpya wa kupanda Mlima Meru kwa kutumia baiskeli, ili kuleta tija zaidi kwenye sekta ya utalii nchini kwa kuongeza watalii na mapato.

Dk Mnaya aliongeza kuwa Hifadhi ya Arusha tayari ina mazingira mazuri na tofauti, hivyo kufikia hatua hiyo wanajipongeza kwa kuanzisha aina hiyo ya utalii na itaongeza wageni watakaofika nchini na mapato.

"Utalii huu katika hifadhi hii unakuwa wa pili baada ya Mlima Kilimanjaro kutumia utalii huu,ila lengo hasa kuvutia watalii zaidi wanaopenda kutumia usafiri huu,"alisema.

Aidha alisema pia zao hilo jipya ni maandalizi ya kukabiliana na wimbi la watalii wengi watakaokuja nchini kutokana na Filamu ya Royal Tour aliyotengeneza Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema katika safari yao watapita vituo vitatu wakitokea geti kuu la Momella ambavyo ni Miriakamba Hut, kituo cha pili ni Saddle Hut na siku ya tatu watafika kileleni katika mlima huo na kushuka.

"Kushuka ni rahisi hivyo watafika geti la Momella walipoanzia siku ya Jumanne ya Mei 10 mwaka huu,"alisema.

Alisema aina hiyo mpya ya utalii itaongeza wageni na kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza hifadhi na kuchangia pato la Taifa.

"Utalii unaofanyika wa kupanda baiskeli hivyo tumejiandaa kuweka usalama kwa wageni wetu pindi wanapopanda mlima huu,"alisema.

Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Catherine Mbena wa kitengo cha Mawasiliano, alisema wameanzisha utalii huo mpya, ili kuhakikisha watalii wanaokuja nchini wanapata ladha mpya kutokana aina ya tofauti za utalii.
 

Kamishana Msaidizi Wa Uhifadhi Anayesimamia Uhifadhi Za Taifa(TANAPA)Bakari Mnaya Akizungumza Katika Uzinduzi Wa Aina Mpya Ya Utali Katika Hifadhi Ya Arusha

Kiongozi Wa Waendesha Baskeli Kuelekea Kilele Cha Mlima Meru Thad Peterson

Afisa Uhifadhi Mwandamizi Wa Shirika La Hi
fadhi Za Taifa (TANAPA) Catherine Mbena  Wa Kitengo Cha Mawasiliano Akiwa Katika Uzinduzi Wa Aina Mpya Ya Utali Wa Baskeli Katika Hifadhi.

Na Mwandishi Wetu Pamela Mollel ,Arusha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments