WAZIRI MKUU ATEMBELEA MAONESHO YA WIZARA YA NISHATI NA TAASISI ZAKE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya Shirika la Petroli Tanzania GASPO - TPDC, Injinia. Bartazar Mroso kushoto) wakati akitembelea mabanda, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nishati, January Makamba, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia vipeperushi, wakati akitembelea mabanda, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, January Makamba, wakati alipotembalea banda la Mkoa wa Kigoma, kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma. Mei 25, 2022.
                * Na Timotheo Kamugisha - Dodoma.*
Watumishi wa Wizara ya Nishati na taasisi zake wamepongezwa kwa kufanikisha wiki ya Nishati iliyofanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma wiki hii.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati alipotembelea kukagua mabanda ya maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Nishati leo Jumatano Mei 25, 2022.

Amesema Waziri wa Nishati alimwambia kuwa ataweka utaratibu utakaowawezesha wabunge kufahamu shughuli zinazofanywa na Wizara ya Nishati kupitia maonyesho ya wiki ya Nishati.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema ubunifu uliofanywa na Wizara ya Nishati ni mzuri kwa kuwa unasaidia kuelewa nini kinaendelea ndani ya Wizara hiyo.

Amesema kuwa wakati akitembelea mabanda mbalimbali amepata fursa ya kutembelea Banda la REA ambayo ina jukumu la kusambaza umeme vijijini ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya umeme.

Amesema kuwa ameona shughuli mbalimbali zinazofanywa na sekta ya Mafuta (TPDC) pamoja na EWURA.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kama yupo mtanzania ambaye hajaelewa Wizara ya Nishati nchini inafanya nini ni vizuri atembelee katika eneo la maonyesho hayo ili apate maelezo ya kina kutoka kwa wataalamu wa Wizara.

Amesema kuwa maonyesho haya yameandaliwa mahsusi kwa ajili ya wabunge, hivyo wabunge watakuwa na nafasi ya kuchangia wakiwa na uelewa mpana nini hasa Wizara ya Nishati inafanya pamoja na sekta zake.

Amesema wabunge wana hamu ya kufahamu umeme utapatikana lini katika maeneo yao, lakini pia kufahamu suala zima la ufungaji waya, eneo la uzalishaji, usambazaji na hatimaye nishati ya umeme kumfikia mlaji.

Amesema ameona mfumo mpya wa kieletroniki unaoonyesha uzalishaji na usambaji namna ambavyo watumishi wa TANESCO wanafanya kazi kwenye vituo vyote vya uzalishaji wa umeme.

Amesema kuna kazi ya kuimarisha Wizara ya Nishati ili iendelee kutelekeza majukumu yake na matokeo yaweze kuwafikia wananchi hasa katika sekta ya Umeme.

Waziri Mkuu Majaliwa amekutana na mameneja wote kuanzia ngazi ya Wilaya hadi kanda na kuagiza watumike kama mabalozi ili waweze kuwaeleza wananchi hatua iliyofikiwa katika sekta ya Umeme.
Na Timotheo Kamugisha - Dodoma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments