Wizara Ya Nishati Yang'ara Maadhimisho Wiki Ya Nishati.

Wabunge wametakiwa kuitumia kikamilifu wiki ya Nishati kupata majibu ya hoja na changamoto za wananchi kuhusu sekta ya Nishati inayojumuisha mafuta, gesi na umeme.

Hayo yamebainishwa kwenye maadhimisho ya wiki ya Nishati iliyoanza katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanzia leo Jumatatu Mei 23 hadi Mei 26, 2022.

Ili kupata majibu ya hoja na changamoto mbalimbali kuhusu nishati, ofisi mbambali zimeandaliwa ikiwemo ofisi ya Waziri wa Nishati, Naibu Waziri wa Nishati, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati pamoja na Wakurugenzi wote wa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema lengo ni kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kupitia maonyesho haya ya wiki ya Nishati hasa kwa wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi.

Amesema kuwa waheshimiwa mabunge watumie maonyesho haya kuuliza na kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalam mbambali kutoka taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Nishati ili kuweza kupata majibu ya maswali ya wananchi wao.

Katika maonyesho hayo wapo wakandarasi wa Miradi ya kusambaza umeme vijijini inayosimamiwa na wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo Waziri Makamba amewataka wabunge kutumia fursa hiyo kuwataka wakandarasi kufikisha umeme katika maeneo ambayo wakandarasi wamechelewesha kufikisha nguzo na kufunga nyanya.

Makamba amesema kuwa moja ya faida ya maonyesho haya pia ni kuwapatia muda wa kutosha wabunge kuuliza maswali yao yote kwa muda wanaotaka katika kipindi hiki cha maonyesho ya wiki ya Nishati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka REA, Julius Budala Kalolo amesema kuwa maonyesho haya ni maelekezo ya Waziri wa Nishati aliyeelekeza kuwa kila mwaka wakati wa kipindi cha Bajeti lazima maonyesho haya yafanyike ili kuwapatia fursa wabunge na wananchi kufahamu maendeleo ya Miradi inayosimamiwa na Wizara hiyo.

Kalolo amesema kuwa miradi mingi inayosimamiwa na REA ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji isipokuwa kuna baadhi ilichelewa kutokana na mchakato wa manunuzi, lakini kwa sasa inaendelea vizuri.

Ametaja kuwa mradi wa mwisho unaosimamiwa na wakala wa Nishati Vijijini utakamilika mwezi Agosti 2023.

Picha Na Matukio Mbali Mbali  Katika Maadhimisho Ya Wiki Ya Nishati













 Na Timotheo Mathayo, Dodoma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments