Wizi miundombinu wamkera Rais Samia


  Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na wizi wa miundombinu ya barabara mpya aliyoizindua ya Tabora hadi Mpanda yenye urefu wa kilometa 342.9 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo leo Jumatano Mei 18, 2022 mjini Sikonge, amesema wanaofanya wizi huo ni wahujumu uchumi.

Ameeleza kuwa baadhi ya watu wameiba taa za barabarani na nguzo katika vijiji vya Kasandalala, Tumbili na Sikonge mjini jambo linaloshangaza kwani miundombinu ni kwa manufaa ya wote.

Mkuu huyo wa nchi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Tabora kuwatafuta wote waliohusika kuhujumi miundombinu ya barabara hiyo ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Awali Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Rogatus Mativila alimweleza Rais Samia kuwa baada ya barabara hiyo iliyojengwa kwa gharama ya Sh473 bilioni kukamilika, baadhi ya watu wameiba taa za barabarani pamoja na alama.

Ameeleza kuwa ilikamilika mwishoni mwa mwaka jana kwa kuwa na alama na Taa za barabarani ambapo baadhi ya watu wameziiba.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments