YANGA HIYOOOOO FAINALI, YAINYOOSHA SIMBA SC 1-0

 Rasmi, Klabu ya Yanga Sc yatinga hatua ya fainali kombe la Azam Federation Cup mara baada ya kuwanyuka mahasimu wao Simba Sc kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.


Bao la Yanga Sc limewekwa kimyani na kiungo matata Feisal Salumu 'Fei Toto kwa shuti kali lililomshinda mlinda lango Beno Kakolanya na kutinga fainali.

Yanga Sc sasa wanawasubiri kati ya Azam Fc ama Coastal Unions ambao watauma hapo kesho katika dimba la Amri Abedi Jijini Arusha.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments