Zuhura Yunus Aeleza Mafanikio Ziara Za Rais Samia Nchi za Nje

Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus amezungumzia mafanikio ya ziara za hivi karibuni alizozifanya Rais Samia Suluhu Hassan nchi za nje.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 12, 2022 Zuhura ameanza na ziara ya kiserikali iliofanywa na Rais Samia Mei 10 na 11 nchini Uganda, akisema ililenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano, pamoja na suala la kiuchumi katika ukuaji wa kibiashara baina ya Tanzania na Uganda.

Katika Ziara hiyo Uganda iliingia makubaliano na Tanzania kuwa italeta tani 10,000 za sukari nchini ili kukabiliana na upungufu wa sukari ambao upo hapa nchini, hata hivyo Takwimu za mamlaka na mapato Tanzania zinaonyesha kwamba mauzo ya bidhaa kutoka Tanzania kwenda Uganda yameongezeka kutoka Sh111.7 bilioni mwaka 2015 hadi ni Sh631.4 bilioni kufikia mwaka 2021.

Tanzania na Uganda wameingia katika makubaliano kwa upande wa gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Uganda, hivyo kuanzia mwaka mpya wa fedha Julai Mosi, Tanzania imekubali kupunguza gharama za usafirishaji wa usafiri wa barabarani hususani malori ya mizigo katika barabara kuu hasa kutoka Mutukula hadi Dar es Salaam.

Amesema katika Sekta ya Afya Tanzania na Uganda wamekubaliana kushirikiana, wakati Uganda teyari wana kiwanda cha kutengeneza dawa za kufubaza Ukimwi ARVS, jambo ambalo katika siku za karibuni Tanzania inampango wa kununua ARVS kutoka nchini Uganda haya yote ni katika kushirikiana na Nchi za Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Sekta ya Nishati kunamakubaliano, kwani kuna hati imetiwa siani ya ushirikiano ya Ujenzi wa kusafirisha umeme ya Kilo Voti 400 kutoka Masaka nchini Uganda hadi Mkoani Mwanza.

Pia ameelezea kuwa, katika ziara ya Marekani ambayo ilianza Aprili 14 hadi 26 mwaka huu, ni kukaribishwa kwa Rais Samia na makamu wa Rais Kamala Harris katika Mkutano uliofanyika Ikulu ya White House Marekani, huku wakizungumzia zaidi jinsi Tanzania inadumisha demokrasia, ukuwaji wa uchumi na mapambano zidi ya Uviko 19.

Amesema Serikali ya Marekani katika suala la biashara na uwekezaji imewaahidi Tanzania kuwa ushirikiano utaendelea, huku wakipendekeza makubaliano ambayo yanaitwa (Open skys Agreement) wakati pande zote mbili zimependekeza kuwe na ndege inayotoka moja kwa moja Marekani hadi Tanzania kwani itaongeza watalii, uwekezaji pamoja na wafanya biashara kwa pande zote mbili.

Kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Zuhura amesema Serikali ya Marekani wamesema wapo tayari kutoa utaalamu wa ushauri kuhusu ujenzi huo wa bandari endapo Serikali ya Tanzania itahitaji, wakati kawa upande wa suala la kisiasa Serikali ya Marekani imeridhishwa na hali ya siasa inavyoendelea hapa nchini

Rais Samia Suluhu pia alikutana na wakuu wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambapo alikutana na Rais wa Benki ya Dunia, David Malpass na kufanya naye mazungumzo, huku banki ya Dunia katika Upande wa Kilimo imeonesha ipotayari kutoa fedha kadhaa, Dola za Kimarekani 120 Milioni ili kufadhili sekta ya kilimo chini ya mradi unaoitwa ASDP2.

Hata hivyo Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani, Kristalina Georgieva amepokea maombi kutoka kwa Rais Samia ambapo, Tanzania imeomba fedha takribani Dola za kimarekani 1.1 bilioni ambazo ni sawa na Sh2.5 trilioni mkopo wa masharti nafuu, ambazo zikipatikana zitakuwa kwa muda wa miaka mitatu.

Amesema kuwa Rais Samia alitembelea taasisi ya Afya inayoitwa SC Johnson ambayo inajihusisha na utafiti wa masuala ya wadudu wanao eneza maradhi mfano Mbu, taasisi hiyo wameonesha kuwa na nia ya kuja kushirikiana na Tanzania na wamekubali kusaini hati ya makubaliano itakayo wezesha Ujenzi wa zahanati kwenye halmashauri zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria, na kuhaidi kuimarisha miundo mbinu katika chuo cha udhibiti wa wadudu wanaodhuru na kueneza magonjwa ambacho kipo Mheza, Tanga.

Kwa kumalizia Royal Tour imeweza kuitangaza Tanzania kwa ukubwa zaidi na kumfanya Rais Samia kuweza kukutana na wawekezaji wakubwa sana katika Sekta za Utali, biashara na filamu ambao wameahidi kuwa wangependa sana kuja Tanzania

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments