ACT Wazalendo Kuongeza Ushiriki Wa Wanawake Katika Siasa

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema chama hicho kitaendelea kuchukua hatua kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya uamuzi vya chama hicho.

Ado ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 4, 2022 wakati akizindua kampeni ya usajili wa wanachama wa chama hicho, kwa njia ya mtandaoni ‘ACT Kiganjani’.

Uzinduzi huo ulikuwa maalumu kwa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo kwa Mkoa wa Dar es salaam na ulifanyika makao ya chama hicho, Kijitonyama.

"ACT Wazalendo inawajali na kuwathamini wanawake. Tutaendelea kuwa mstari wa mbele kuboresha ushiriki wa wenu kwenye vyombo vya maamuzi ndani na nje ya chama kwa kuweka mazingira mazuri ya kisheria, kisiasa na kijamii,” amesema Shaibu.

Hata hivyo, Shaibu amewataka wanawake wa chama hicho, kusimama imara na kupigania kila fursa inayojitokeza akisema shughuli za kisiasa ni uwanja wa mapambano.

Amesema hivi karibuni chama hicho, kitafanya uchaguzi wa uongozi mpya wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuvunjwa kwa uongozi uliokuwepo.

Nitafarijika sana iwapo wanawake wengi zaidi watajitokeza kugombea. Ndani ya ACT-Wazalendo wanawake wana fursa ya kugombea nafasi yoyote kwa mujibu wa Katiba na Kanuni,” amesema Shaibu.

Katika hatua nyingine, Shaibu ameitaka ngome ya Wanawake ya Mkoa wa Dar es salaam kushirikiana na msemaji wa sekta ya Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupigania maslahi ya wanawake katika mkoa huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments