BAJETI YA SERIKALI IMEAKISI DHAMIRA NJEMA YA RAIS SAMIA KWA WATANZANIA...TUSHIRIKIANE KUFIKA 'NCHI YA AHADI'

 Nikiri mapema binafsi nimevutiwa na Bajeti Kuu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imewasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Mwigulu Nchemba.


Katika bajeti ya mwaka huu wa 2022/2023 imepanga kutumia Sh.Trilioni 41.4, kwangu ambalo limenifurahisha naamini na wengine wamefurahi ni namna ambavyo bajeti ilivyoakisi nia njema ya Serikali katika kuwaondoa Watanzania walio wengi kwenye lindi la umasikini. Ndio....,ukisoma bajeti unaona nia njema ya Serikali, imedhamiria kuleta maendeleo.

Nafahamu bado kama nchi kuna maeneo yanahitaji kuwekezwa zaidi ili kufika kule ambako tunataka kwenda na hasa kwenye kuhakikisha changamoto tulizonazo zinapatiwa ufumbuzi

Jambo jema kwenye bajeti ya mwaka huu imejibu maswali mengi ya jinsi gani changamoto hizo zitaondolewa na naamini Serikali ya Rais Samia hakuna kinachoshindikana.., Ndio hakuna kinachoshindika kwasababu tangu ameingia yote yaliyokuwa yameshindikana kwake ameendelea kuyapatia ufumbuzi.

Ngoja nikwambie kitu bajeti ya mwaka huu imegusa maeneo mengi na yote muhimu lakini lazima tukiri eneo la kilimo limebeba kundi kubwa la Watanzania ambao wanajihusisha na shughuli za kilimo.
Kwenye bajeti hiyo imeeleza hatua kwa hatua ambavyo imejipanga kuimarisha sekta ya kilimo ili kiendelee kuwa na tija zaidi ya ilivyo sasa.

Ukisoma bajeti hiyo inaonesha kwamba katika kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji na zinazotengeneza ajira kwa vijana, Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia imeongeza bajeti ya Kilimo kutoka shilingi billion 294 hadi shilingi bilioni 954 na itaendelea kuongezeka kila mwaka.

Naamini lengo la Serikali ni kuhakikisha sekta ya kilimo inakua kwa zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Bajeti ya mwaka 2022/23 ni msingi muhimu kufikia lengo kuu hilo.

Kupitia bajeti hiyo inaelezwa kwamba Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Samia inalenga kutengeneza ajira kwa vijana na wanawake zaidi ya milioni tatu katika sekta ya kilimo ifikapo mwaka 2025.

Kwa dhamira hiyo njema ya Serikali ya Rais Samia nakwenda kubadilisha maisha ya watanzania walio wengi ambao wanajihusisha na kilimo.
Tumekuwa tukielezwa kwa Tanzania kilimo ndo UTI wa mgongo na Serikali kwa kuendelea kutambua hilo imeamua kuweka nguvu katika kilimo.

Ukiondoa kilimo eneo lingine ambalo nimevutiwa nalo na linagusa maisha ya walio wengi ni kwenye sekta ya uzalishaji na ajira kwa vijana. Taifa letu ni Taifa la Vijana, (wastani wa miaka 18). Miaka ya sitini, miaka ya sabini na miaka ya themanini vijana walikuwa wanahudumia wazee na watoto. Njia ilikuwa rahisi kwa wahitimu wakitafutwa wangali masomoni wachague wanataka kwenda kufanya kazi taasisi gani.

Hali haiko hivyo sasa kwani hivi sasa, wazee ndio wanahudumia vijana na watoto wao.
Ni kawaida sasa kukuta mzee wa kijijini au mstaafu akiwahudumia vijana wahitimu. Uwiano huu sio mzuri kwa Taifa letu kuwa na nguvu kazi kubwa ambayo haiko kazini licha ya uwekezaji mkubwa uliowekwa katika sekta za uzalishaji.

Kutokana na changamoto hiyo Serikali ya Rais Samia imefafanua kwa kina mipango yake sasa na Sera zake kwmba lazima zijibu mahitaji ya vijana wa Tanzania.

Mbali na eneo la uzalishaji Serikali ya Awamu ya Sita imetangaza kuwa katika elimu pamoja na mambo mengine imetenga fedha kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa kidato cha Tano na Sita.Hivyo uamuzi huo unakwenda kuifanya elimu ya kuanzia elimu msingi hadi kidato cha Sita kutolewa bure.Huyo ndio Mama Samia,mama mwenye upendo wa kweli.

Katika bajeti ya mwaka huu , Serikali inaeleza kuwa itaendelea kugharamia programu ya elimu msingi bila ada ambapo hadi Aprili 2022, jumla ya shilingi bilioni 244.5 zilitolewa.

Ngoja nikwambie Mtanzania mwenzangu, Rais Samia ameguswa sana na watoto kukatisha masomo kwa ajili ya sababu mbalimbali. Miongoni mwa sababu zinazosababisha kukatisha masomo ni umaskini wa kipato kwenye familia zetu.

Sababu nyingine ni mimba za utotoni, mwamko duni wa elimu kwa baadhi ya jamii na utoro na wale wasioendelea kufuatana kwa mujibu wa sheria (Ufaulu). Ili kukabiliana na utoro (drop out) wa wanafunzi wanaotoka familia maskini, bado kuna watoto wanaoshindwa kumudu mahitaji ya lazima licha ya kuwepo kwa programu ya elimu bila malipo.

Kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya Fedha ni zaidi ya Shilingi Bilioni 10 (10,339,350,000).

Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Rais alivyoielekeza Wizara, kufuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita.Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita.

Hakika kwenye eneo hilo elimu bure narudia tena kwa msisitizo hongera Serikali ya Awamu ya Sita, hongera kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua hii ya kuona umuhimu wa Watoto wa nchi hii kupata elimu bila vikwazo hasa vinavyohusu fedha.a

Tunafahamu juhudi ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Serikali katika eneo la elimu, sitaki kuzungumzia ujenzi wa madarasa zaidi ya 17000 ya Sekondari.Ujenzi huo imefanyika kupitia fedha za UVIKO-19 ambazo zilitolewa na Rais Samia.Ni Kwa mara ya kwanza vijana waliofauli darasa la Saba wote wamekwenda sekondari.

Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ya miaka mingi ilikuwa kwenye changamoto ya uhaba wa madarasa na hivyo wanafunzi wengi hawakuweza kujiunga na masomo ya Sekondari kwa wakati.Rais Samia ameondoa changamoto hiyo lakini kwa mapenzi yake mema na Watanzania amewaondolea adha nyingine ya ada.

Kwa nyakati tofauti Rais Samia amekuwa akizungumza kuhusu dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Watanzania katika kuleta Maendeleo.Sote tunafahamu ili Taifa lolote lipige hatua lazima liwekeze kwenye elimu.

Hivyo Rais Samia ameona haja ya kuweka nguvu zake kuboresha mazingira ya elimu yetu. Watanzania watakubaliana nami utoaji wa elimu bure Rais anakwenda kugusa maisha ya walio wengi hasa wenye vipato vya chini

Kwa upendo huu wa Rais Samia, kwa Wema wake huu kwa Watanzania wote kwa umoja wetu tunakila sababu ya kuungana na kumpongeza na kumuombea afya njema.
Anayoyafanya tangu ameingia madarakani yanagusa maisha ya walio wengi.Hongera Rais Samia.

Jukumu limebaki kwa wasaidizi wa Rais Samia kutekeleza Yale yaliyopangwa kufuatana na bajeti ya mwaka huu iliyosonwa Dodoma wiki hii.Na kwetu wananchi njia pekee ya kuunga mkono juhudi hizi za Rais Samia na Serikali yake katika kututoa hapa tulipo na kutufikisha 'nchi ya hadi' ni kuhakikisha tunashirikia kikamilifu kwenye shughuli zote za maendeleo.

Pamoja na hayo tunafamu maendeleo ya Watanzania yataletwa na sisi wenyewe kwa kushiriki kwenye hatua mbalimbali za ujenzi wa Taifa hili na ili hayo yote yafanyike ni lazima tulipe Kodi.Kwenye hili la kodi nimeona mkakati wa Serikali.

Imetoa maelekezo ya jinsi gani kila Mtanzania atalipa kodi na njia mojawapo ni kuanzishwa kwa utaratibu wa Namba ya mlipa kodi.Na Serikali itaweka utaratibu wa kila mwananchi anayeanzia umri wa miaka 18 awe amesajiliwa kwa maana ya kuwa namba hiyo ya mlipa Kodi.

Ni wajibu wote kuunga mkono utaratibu huo hasa kwa kutambua tunayo nafasi ya kuwa sehemu ya kuchangia kwa maendeleo yetu.Katika hili la kulipa Kodi naomba nieleweke wale wote wanaofanya shughuli zao halali watambue wanayo nafasi ya kulipw kodi kwa maendeleo ya Taifa letu .

Nihitimishe kwa kurudia tena kueleza hivi kupitia bajeti hii ya Serikali inaonesha mwanga wa tumaini jipya la Watanzania katika kujivunia nchi yao ambayo inaangalia Dunia kwa jicho la kimaendeleo.Nihitimishe kwa kueleza hivi pamoja na Bajeti yetu nzuri, Rais Samia ameendelea kuifungua nchi yetu kwa kuonesha fursa zilizopo ambazo wawekezaji wanaweza kuja kuwekeza nchini kwetu.

Ndio maana yuko kwenye ziara ya kikazi Oman na huko ameshuhudia utiwaji saini mikataba mbalimbali ikiwemo ya wanaotaka kuja kuwekeza.Ahsante Rais Samia.Watanzania tuko pamoja na wewe.Tunakuunga mkono kwa maslahi maana ya nchi yetu.Post a Comment

0 Comments