BASI LA ZUBERI LAUA WATU WATATU, KUJERUHI BAADA YA KUGONGA DARAJA MWIGUMBI

Watu watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga.

 

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga ambapo basi hilo lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA liligonga ukingo wa daraja la Mwigumbi na kutumbukia bondeni.


Kamanda Kyando ametaja mmoja wa waliofariki dunia kuwa ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.


Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.


Aidha, ametoa wito kwa madereva kuchunguza afya zao kabla ya kuanza safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments