CCM KUFANYA TATHMINI YA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA HALMASHAURI NCHINI.

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitafanya tathmini ya kina kuona kama halmashauri zote nchini zinatenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kama sheria inavyoelekeza kwa ajili ya mikopo isiyo na riba na kama fedha hizo zinawafikia wanufaika ambao ni Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu.


Hayo yamesemwa leo Jumamosi Juni 04, 2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM-Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na mamia ya Wananchi wa Kijiji cha Namtumbuka kwenye Wilaya ya Mtwara Vijijini kwenye mwendelezo wa ziara yake ya siku 4 mkoani Mtwara.

Shaka amesema kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu mikopo hiyo kwa baadhi ya Halmashauri nchini kutenga fedha kidogo na walengwa kutopata fedha hizo.

"Kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) tutafanya tathmini kuona kama fedha hizo zinatengwa kwa mujibu wa sheria na walengwa wa mikopo hiyo wananufaika. Yapo maeneo fedha hizi zimekuwa zikiliwa na baadhi ya watumishi wa serikali na viongozi wasio waaminifu kwa mgongo wa kutengeneza vikundi feki.

Aidha Shaka amesema ikibidi Chama kitaishauri Serikali kuona namna nzuri zaidi ya mikopo hii kuwanufaisha walengwa." Alisema Shaka.

Shaka alilazimika kuyasema hayo wakati akijibu swali la Bi. Ashura Mbose aliyetoa kero ya kutopata mikopo hiyo ya Halmashauri Kijijini kwao Namtumbuka.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments