CCM YAVIELEKEZA VYOMBO VYA DOLA KUCHUKUA HATUA KWA WAFANYABIASHARA WANAOHUJUMU MPANGO WA WAUGAWAJI PEMBEJEO.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mtwara kutomfumbia macho na mfanyabiashara wa pembejeo anayetumia vibaya jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika biashara yake ya pembejeo feki za kilimo.

Shaka ameyasema hayo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara, ambapo amesema mfanyabiashara huyo anauza pembejeo zisizokidhi viwango huku akidai ni mali ya Waziri Mkuu Majaliwa jambo ambalo sio kweli.

Amesema mfanyabiashara huyo anafanya hujuma dhidi ya juhudi za rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wakulima ambapo serikali inagawa bure pembejeo hizo.

"Na bahati mbaya sana mfanyabiashara huyo anatumia jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba eti hiyo ni mali ya Waziri Mkuu na yeye amepewa uwakala na Waziri Mkuu. Vyombo vya ulinzi na usalama huyo mtu bado yupo tu mtaani kweli!.

"Kweli huyo mtu bado yupo tu mtaani, sijui kwa sababu ana nguvu ya fedha sijui kwa kweli, na bahati nzuri nilipopata taarifa na nikapata ushahidi nilimtafuta waziri Mkuu, nikamwambia mheshimiwa waziri Mkuu, akaniambia katika hili huyo mtu aje athibitishe.

"Sijawahi kufanya biashara ya pembejeo si Mtwara, sio sehemu yoyote sihusiki na hilo jambo na mie nashangaa vyombo vya ulinzi na usalama havijamtia mkononi bado, na anasambaa ndani ya Mkoa huu wa Mtwara," amesema.

Kwa mujibu wa Shaka ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, amesema miongoni mwa wahusika wa mchezo huo mchafu wa biashara ya pembejeo feki, wamo baadhi ya madiwani ambapo ameisitiza kuwa Chama hakitamvumilia kiongozi yeyote atakayethibitika kufanya uhalifu.

Aidha Shaka amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani huko kuhakikisha wanasimamia zoezi la usambazaji wa pembejeo hizo na kutekeleza dhamira njema ya Rais Samia kwa wananchi
 

Post a Comment

0 Comments