CHONGOLO AMTAKA MBUNGE WA ITILIMA KUHAKIKISHA KILA TARAFA INAPATA MASHINE YA KUSUKUMIA ALIZETI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amemtaka mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga kuwawezesha wakulima wa Jimbo Hilo kuhakikisha Kila tarafa wanapata Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti Ili kuongeza thamani ya zao hilo ambapo kwa Mkoa wa Simiyu, Itilima inaongoza kwa uzalishaji wa alizeti.


"Najua Mbunge wenu ana wajibu wa kuwasaidia mashine za kuchuja mafuta ya alizeti, wasaidie wananchi Hawa wapate mashine za kuchuja mafuta ya alizeti angalau kwa mashine moja kwa Kila tarafa na hili litawasaidia sana kuongeza thamani ya zao hili."

Katibu Mkuu ameongeza kuwa kitendo Cha kufunga mashine, wakulima wataanza kuuza mafuta badala ya kuuza alizeti zenyewe, ambapo kwa sasa mafuta ya alizeti ndio mafuta bora na ghali zaidi, hivyo wananchi watapata fedha za kutosha tofauti na sasa.

Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 2 Juni, 2022 alipowasili Wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu wakati akiendelea na ziara yake yenye lengo la kukahamasisha uhai wa Chama ngazi za mashina na Kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.













Post a Comment

0 Comments